KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSI YETU?
SIMULIZI YA KWELI
1-------5
KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSI YETU.
Ulikuwa ni usiku wao wa kwanza .John alifunga mlango wa chumba chao kwa funguo kisha akaelekea msalani huku akimuacha bibi harusi akiwa kitandani akiperuzi simu .Alinawa uso na kutoka.
Ile anatoka chooni alishtuka kumkuta bibi harusi akiwa amechomwa kisu kifuani na kulala kitandani.Alimsogelea na kumtikisa akagundua ameshaaga dunia.Aliangalia kushoto na kulia hakuona mtu.
Alienda kuangalia mlangoni alikuta mlango umefungwa kama
alivyouacha.Kichwa kikamuuma.Alijiuliza nani
aliyemchoma kisu mke wake katika siku ya fungate.Alitamani kupiga kelele lakini halijizuia.
" hivi nini kinachoendelea.Yaani dakika moja niliyoingia chooni mtu aingie na kumuua mke wangu.Mbona sijasikia kelele yeyote? Mbona mlango upo vilevile kama nilivyoufunga,mbona dirisha limefungwa vile vile?,Mbona kila kitu kipo vile vile? Inawezekana vipi? " alijiuliza maswali bila majibu.
Alikaa chini na kuiangalia maiti ya mkewe iliyokuwa imelala kitandani.Damu zilichuruzika na kuchafua mashuka.Alipoisogelea maiti vizuri aligundua kisu alichochomwa
mke wake ni kisu ambacho yeye alikitumia kukatia tikikiti barazani.
Moyo wake ulivuja damu kwa uchungu.Akajikuta anashindwa kuvumilia akaanza kulia kwa uchungu.Kilio chake kiliwashtua ndugu zake ambao walikuwa wanaburudika barazani kusherekea harusi yao.
" mmmmh mbona kama shem analia,kuna nini?" aliuliza dani .
Waliangaliana pale barazani kwa dakika kadhaa kisha wakaamua kukimbia kwenda kuangalia.Walifika mlangoni wakagonga ili john awafungulie lakini john hakufungua.Aliendelea kulia mle ndani kwa sauti kubwa.
Hofu iliwajaa pale mlangoni wakajaribu kufungua mlango,lakini walishindwa.Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.
"Shem fungua mlango.Kuna nini shem hebu fungua mlango" aliongea dani.
John kwa unyonge huku akilia aliusogelea mlango na kuufungua.Haraka sana wakaingia mle chumbani.Kufika mle ndani wote walishikwa na butwaa baada ya kumuona bibi harusi akiwa amechomwa kisu kifuani .
"Aaaah dadaaa,dadaaaa " aliita dani huku akimsogelea dada yake na kuanza kumtikisa kwa nguvu.
"Kwanini umemuua dada yangu? Amekukosea nini?" alifoka dan.
" hapana ,sijamchoma mimi,sio mimi " alijitetea john.
Ndugu wote mle ndani walishikwa na butwaaa.Wote walimlaumu john kwa mauaji ya bibi harusi,ambae ni mke wake.Maelezo aliyoyatoa kuwa ametoka chooni na kumkuta mke wake akiwa ameshakufa hakuna aliyeyaelewa.
" acha kutufanya sisi watoto? Humu ndani mlikuwa wawili tu,sasa nani mwengine amchome kisu dada kama sio wewe.Na mlango ulifunga " alifoka dani na kumvaa shemeji yake.
" Nakuua leo ,nakuuua ,kama ungekuwa haumtaki si ungesema.Kwanini umemfanyia hivi,unakataaa wakati kisu ulichomchoma nacho ulikishika mwenyewe ata kule barazani nilikuona nacho" aliongea dan.
John alijaribu kujitetea lakini hakuna aliyemwelewa .
" mwanangu kwanini umefanya hivi? Amekufanya nini mtoto wa watu?" mama yake john alimuuliza mwanae huku akitokwa na machozi.
"Mama sijamuua mimi? Sio mimi mama" alijitetea john
" kama sio wewe ni nani? Ona sasa utaenda kuishi gerezani na kuniacha peke yangu.Bila wewe nitafanya nini mimi?" aliongea mama yake john na kuanza kulia kwa nguvu.
Ndugu wa bibi harusi walishindwa kuvumilia.Walimvamia John na kuanza kumpiga.Walimpiga sana,ndani ya muda mfupi alikuwa amechakaa, sura nzima ilikuwa imetapakaa damu.
" mwachane jamani,mwacheni msimfanyie ivyo.Mtamuua na nyie mtapata matatizo,mwchenii.Nimewapigia polisi wanakuja kumchukua" aliongea mjomba wa bibi harusi aliyeuwawa.
Haikuchukua muda polisi wakafika na kumchukua john.Walimfunga pingu na kuondoka naye.Akiwa kwenye defender anapelekwa polisi,kichwa chake bado kilikuwa kwenye mawazo mengi.
Alikuwa anawaza ni nani,aliyefanya ule unyama.Na aliweza vipi bila kufungua mlango wala dirisha.
" chooni nilikaa dakika moja tu,mlango hukufunguliwa?,dirisha alikufunguliwa ,sasa nani kafanya vile? iliwezekana vipi?" aliwaza john,
Ndimi
Mjamaa samwely kisinga Msendembali songea.
KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSI YETU - 02
Tulipoishia - Alikuwa anawaza ni nani aliyefanya ule unyama.Na aliweza vipi bila kufungua mlango wala dirisha.
" chooni nilikaa dakika moja tu,mlango hukufunguliwa?,dirisha alikufunguliwa na ndani ya muda mfupi vile iliwezekana vipi?" aliwaza john,
Endelea nayo.
Mawazo yalimzonga john.Alijaribu kungamua lile tukio lakini hakupata majibu.Kifo cha mwanamke anayempenda sana katika siku ya fungate kilimchanganya,lakini kilichomchanganya zaidi ni tukio jinsi
lilivyotokea.Hakuwa na majibu ,alihisi labda ni muujiza flani.
" mmmmmh! Au sara alijichoma kisu mwenyewe?, mmmh hapana haiwezekani? Kwanini ajichome kisu. Mbona muda wote wa sherehe alikuwa na furaha tu.Haiwezekani akawa amejiua mwenyewe" aliwaza john
Akiwa kwenye mawazo alishituliwa na teke alilopigwa mgongoni.
" hebu simama telemka haraka" alifoka askari huku akimpiga mateke john kumtaka ashuke kwenye gari.
John aliangaza macho kushoto na kulia akagundua wameshafika kituoni.Njia nzima akili yake ilikuwa kwenye
mawazo mazito,hivyo akujua kama wamefika.Alishuka kwenye gari na moja kwa moja akaingizwa kituoni.
Polisi waliandika andika kisha wakamwambia atoe maelezo yake.John alieleza kila kitu kama kilivyotokea.Polisi hawakumuelewa ,wakawa wanamlazimisha akubali kuwa yeye ndiye aliyemuua mke wake .
" acha upumbavu wewe jamaa.Chumbani mlikuwa wewe na bibi harusi tu.inakuwaje unakataa kuwa sio wewe? Kama sio wewe basi unataka kusema bibi harusi alijichoma kisu yeye mwenyewe?" alifoka askari huku akimtikisa john kwa nguvu.
" kweli mimi sijamuua mke wangu? Kwanza nampenda.Kwanini nimuue mtu ninayempenda.Sara ni mpenzi wangu,tena ni mtu ninayempenda kuliko kitu chochote ,kamwe siwezi kumdhuru mke wangu mimi mwenyewe.Haiwezekani kabisa" aliongea john.
" unajifanya kiburi,sasa kwa taarifa yako utaongea tu.Wauaji wote wakijaga hapa uwa wanakataa lakini mwishoni uwa wanakubali makosa yao.Sasa ngoja nikupe ushauri wa bure.Ni vyema ukakubali kabisa saizi kabla hatuja uvunja vunja mwili wako" aliongea yule polisi aliyeenda kumkamata.
" afande! Kama kunitesa ,niteseni tu.ila ukweli ndio huo.Mimi sijamuua mke wangu.MKe wangu nampenda sana,siwezi kumfanyia ukatili kama ule" aliongea john.
Polisi walimtisha sana lakini john aliendelea kukataa.Walimchukua na kumtupa sello.John aliingia mle sello na kwenda kuchuchumaa kwenye kona moja ya kile chumba.Mle ndani mlikuwa na watu wengi sana.Wengi walikuwa na makovu mengi sana usoni.
John ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukamatwa na kuwekwa sello.Maisha yake yote alikuwa hajawahi kumshitaki mtu polisi wale yeye alikuwa hajawahi kwenda polisi kushtakiwa.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza.
Mazingira ya mle ndani yalimtisha.Woga ungamwingia.Kila aliyemuangalia alimuona sio mtu wa kawaida.Kumbukumbu ya tukio la kifo cha mkewe na hali mbaya ya mle ndani ilimfanya machozi yamtoke.Taratibu machozi yakawa yanatirirka kwenye mashavu yake.
Kitendo chake cha kulia kiliwakera watuhumiwa wengine waliokuwa mle ndani.
" aaah! Huyu jamaaa vipi? Yaani ameingia leo halafu analia kama mtoto wa kike bwana.Washikaji huyu sio bure,huyu atakuwa bwabwa tu" aliongea hamisi ,Maneno yake
yaliwafanya wenzake wacheke kwa nguvu.
" oya acha uboya wewe.Mambo gani haya?, unaliaje kama mtoto wa kike?" hamisi alimsogelea john na kumtikisa.Kitendo cha john kushikwa na kutikiswa kilifanya hofu izidi kumwingia .
" kwanza umefanya kosa gani? Kosa gani lililokuleta hapa" alimuuliza
" mi mi ,sija.... Sija.....ni....??" john alishikwa na kigugumizi,akashindwa kuongea.
"Usiogope mtoto mzuri.Sema umefanya nini mpaka umeletwa huku"
aliongea kulwa huku akimpiga piga mgongoni .
" wamenizingizia nimemuua mke wangu,lakini mimi sijamuua ,nimemkuta amekufa" aliongea john.
" aaah! Wamekuzingizia?, daaah hawa polisi sio watu wazuri kabisa.Yaani hata sisi wote humu ndani wametuzingizia" aliongea kulwa.Kauli yake ya kusema wote wamezingiziwa iliwafanya wafungwa wote wacheke mle ndani.
Kulwa sura yake ilikuwa na makovu mengi ya mapanga .Alikuwa ni jambazi mzoefu.Kutokana na sura yake kutisha sana,John aliingiwa na hofu zaidi.
Haukupita muda mrefu polisi waligonga mlango wa sello wakamtoa nje.Mama yake alikuwa amefika kumuona.
"John mwanangu,kwanini umenifanyia hivi mimi? Unajua wewe ndio mwanangu wa pekee.Wewe ndiye ninayekutegemea,bila wewe nitafanya nini mimi?" aliongea mama yake john ,huku machozi yakimtoka.
" eeeh eeeh wewe mama kelele zako ziondoe hapa!.Hakuna msiba hapa" alifoka polisi.
" na kama unalia lia namrudisha huyu selo.Nimekubali uongee nae ili umshawishi akubali na sio wewe kulia lia"
" hapana naomba msirudishe ndani,naomba mnisamehe" aliomba samahani mama john huku akifuta machozi.Waliingizwa kwenye chumba flan wakaachwa waongee.
" mwanangu mimi mama yako?, niambie ukweli,kwanini umemuua mkeo kikatili vile?"
" Hapana mama!,mimi sijamuua, nimetoka bafuni nikakuta ameshakufa."
"Hivi unazani kuna mtu anaweza kukuelewa.Kwa mazingira yalivyo wewe ndio muuaji.Ni bora ukakubali mapema labda unaweza kupunguziwa adhabu "
" aaah mama! Nitakubali vipi kitu ambacho sijakifanya.Naanzaje kukubali kuwa nimemuua mke wangu wakati sio kweli.Hapana mama siwezi kukubali kabisa" aliongea john.
Mama yake alijaribu kumshawishi lakini john aliendelea kukataa.Askari walimchukua na kumrudisha sello.Polisi na jamii kwa ujumla waliamini kuwa john ndie aliyemuua mke wake.Kuendelea kwake kukataa kulimuuzi askari ambae alipewa kesi aipeleleze.Alimchukua john na kumuingiza kwenye chumba cha mateso.
" kwakuwa umeshindwa kukubali mwenyewe kwa hiari yako.Sasa
nitakufanya ukubali kwa lazima." aliongea afande mwita huku akimvua nguo John.Alimvua nguo zote na kumuacha uchi kama alivyozaliwa.
Kwakushirikiana na askari mwenzake walimkamata na kumfunga kwenye kiti.Alichukua koreo na kubana korodani za john. John alipiga kelele.Walimziba mdomo na kuendelea kumtesa.Maumivu aliyoyasikia yalikuwa hayaelezeki.
Wakiwa wanamtesa mlango ulifunguliwa aliingia afisa upelelezi .
" Huyu jamaa wa ajabu sana.Yaani anakataa wakati kila ushahidi unaonyesha muuaji ni yeye?, nimetoka kuchukua majibu ya fingerprints
zilizokuwa kwenye kisu.Majibu yanaonyesha finger prints zilizokuwa kwenye kisu ni za kwake" aliongea yule afisa upelelezi.
Taarifa ile ilikuwa mwiba mkali moyoni kwa john.
" aaah yaani hadi fingerprints zinaonyesha ni mimi? Inawezekana vipi? Mbona nilikuwa chooni" aliwaza john.
Ndimi
Mjamaa samwely kisinga..
KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSI YETu - 03
Tulipoishia - Taarifa ile ilikuwa mwiba mkali moyoni kwa john.
" aaah yaani hadi fingerprints zinaonyesha ni mimi? Inawezekana vipi? Mbona nilikuwa chooni" aliwaza john.
Endelea nayo.
Akiwa anawaza ayo alipigwa makonde mazito usoni mfululizo.Sura yake ilijaa damu.
" jamanii sijaua mimi ,Afande mnanionea" alilamika john.Maneno yake yalimtibua yule mpelelezi.Alikipiga kiti teke john akaanguka mzima mzima.Akiwa
ameanguka chini afande alitoa mkasi akauweke kwenye sehemu zake za siri.
" nikate hiii au utasema" alimuuliza john.John alitoa macho kwa mshangano,afande akabana mkasi taratibu ,hali ilyopelekea john apige kelele kwa nguvu.
" nitasemaaa ,nitasemaaa usinikate" aliongea john,
" aya nimetoa mkasi sasa.Hebu sema haraka kwanini umemuua mke wako kikatili vile"
" aaah....ee.....a......as......"
" pumbavu wewe.Hebu sema haraka kabla sijazikata hizi.Hivi unaleta mzaha sio?"
" Hapana afande ,sileti mzaha.ile ukweli ni kuwa mimi sijamuua mke wangu.Kwanza bado nampenda sana.kifo chake ata mimi kimeniuma sana"
" Pumbavu,sijakupa nafasi ya wewe kuniambia unampenda mke wako.Nafasi niliyokupa niyawewe kukiri kosa.sasa kwakuwa unajifanya kiburi ngoja nikuoneshe" aliongea yule afande kisha akashika uume wa john na kuanza kuuvuta kwa nguvu.
Maumivu aliyoyasikia john yalikuwa hayaelezeki.Alilia na kupiga kelele kama mtoto mdogo.
" utaniuuua,unaniuuua" alipiga kelele john,lakini yule askari hakumuelewe aliendelea kuzivuta tu.John macho yake yakaona giza mbele yake,pale pale akazimia.
" unajifanya umezimia ili ukimbie mateso.aaah wewe mpumbavu kweli.Ngoja nikuoneshe" aliongea yule askari kisha akachukua ndoo la maji na kummwagia john.Alimwangia maji kisha akamtikisa kwa nguvu.Baada ya kutikiswa kidogo fahamu zake john zikarejea.
Baada ya fahami kurejea yule askari alichukua koreo na kubana sehemu zake za siri tena." aya utasema au hautasema? " aliuliza yule afande.
Maumivu akiyoyapata john yalikuwa ni makubwa kupita maelezo.Moyoni mwake alishakata tamaa.
" mmmmh! Hapa nitakufa huku najiona.Ni bora nikubali tu ili yaishe.Kwakuwa wao wanaamini ni mimi.Hata nikikataa vipi haina mana.Japo sijaua mimi ngoja nikubali tu ili niepuke aya mateso " aliwaza john moyoni.
" nimekubaliii nimekubaliii, ni mimi ndie niliyemuuua" aliongea john huku
machozi yaliyochanganyika na damu yakitiririka kwenye mashavu yake.
" mambo si hayo,sasa ungesema mapema mbona hizi tabu zote usingezipata" aliongea yule askari huku akimfungua john kwenye kile kiti.
.....................rn
Baaada ya taratibu za kipolisi kukamilika mwili wa marehemu sara ulikabidhiwa kwa ndugu zake ili wakauzike.Ndugu waliamua wausafirishe wakauzike kijijini kwao mapogoro mkoani iringa.
Taratibu zote zikafanyika.Wakakodi magari mawili,moja basi kwa ajili ya kusafirisha watu na lingine ni gari
ndogo kwa ajili ya kubeba maiti ya sara.Nduvu wa john walifika kuhudhuria msiba.Mama yake john muda wote alikuwa akilia huku akimuomba marehemu amsamehe mwanae kwa kile alichomfanyia.
" halafu hawa ndugu wa john wamefata nini hapa?,Ndugu yao amemuua dada yetu kikatili vile halafu wao wanajifanya kuja tena" dani alimwambia mdogo wake aitwae respiqus.
" aaah brooo achana nao.Aliyemuua dada ni ndugu yao ,na wala sio wao.Hivyo sio vizuri kuwahukumu wao kwa makosa ya ndugu yao"
" daaah! Dogo kumbe na wewe unaroho mbaya sana.Sikutegemea kama unaweza kuongea ayo.Aliyeuwawa ni dada yetu.Tena ndio dada yetu wa kwanza katika hii familia.Wazazi wetu wametumia hela nyingi sana kumsomesha,lakini kabla hata hawajala matunda yake ,anatokea mpumbavu flan anamuua halafu wewe unataka nikae kimya,hapana .ilo haliwezekani,naenda kuwatimua" aliongea dan huku akiwasogelea ndugu wa john.
Mdogo wake respiqus alijaribu kumzuia lakini ilishindikana.Dan alienda hadi kwa mama yake john ambae alikuwa akilia muda wote.
" Acha unafiki wewe mama. Mumemuua dada yetu halafu unajifanya kujiliza hapa Naomba toka nisikuone hapa.Tokaaa haraka sana kabla sijakufanya kitu kibaya" alifoka dan.
Watu walimfata dan na kujaribu kumtuliza lakini ilikuwa ni ngumu.Mama john hakuondoka aliendelea kukaa pale pale.Hali ile ilimtibua dan,upesi akaingia ndani kuchukua panga.
" unajifanya hutaki eeh! Sasa ngoja nikuoneshe" alifoka dan huku akimsogelea mama john na upanga.
Kuona vile ndugu walimuwahi na kumzuia.Wazee wakamshauri mama
john na ndugu wengine wa john,waondoke eneo lile.Mama yake john alikubali ,taratibu yeye na wenzake wakaanza kuondoka.
" ona mwanangu ulivyonidhalilisha.Kwanini lakini john umefanya hivi?" aliongea huku akifuta machozi mama john.
Taratibu zote za kusafirisha mwili zilikamilika.Wakawa wanapanga watu wa kusafiri hili waweze kuondoka.
" itabidi majirani wawili waende kuwawakilisha wenzao.Haiwezekani tukaenda ndugu tu" aliongea mjomba wake sara.
" sasa sijui ni jirani yupi na yupi watakaokubali kwenda." aliuliza shangazi yake sara.
" mmmh! Majirani wako wengi.Wewe watangazie tu,ukiwatangazia nani yuko tayari kwenda wenyewe watajitokeza "
" sawa ngoj nifanye ivyo" aliongea shangazi yake sara na kuondoka kuelekea ndani.
Alienda moja kwa moja walikokaa majirani na marafiki zake marehemu sara." jamani kuna nafasi mbili tu za majirani kwenda ,sasa sijui ni nani na nani wataenda kati yenu?" aliwauliza.
" mmmmh! Mnachotaka kukifanya sio kizuri!,haiwezekani waende wawili
tu.Sara alikuwa anaishi vizuri sana na watu hapa.Mimi nilikuwa nashauri waende angalau watano."
" aaah! Watu watano haitawezekana.Gari limeshajaaa."
" kama limejaa sisi tutakuja na gari letu,maana haiwezekani yaani tusiende kumzika mwenzetu kisa kujaa kwa gari" aliongea mwajuma,ambae alikuwa ni shoga mkubwa wa sara.
" kama ivyo sawa.Ngoja nikamwambia mzee mkoroma." aliongea shangazi yake sara kisha akasimama kuelekea walikokuwa wamekaa wazee.
" samahani mzee nakuomba mara moja"
" sawa ,nakuja" alijibu mzee mkoroma kisha akasimama kumfata.
" aya niambie.mmmmh! Lakini kabla hujaniambia uliloniitia,na mimi nina jambo nataka nikuulize"
" mmmmh! Jambo gani tena ilo mzee! "
" ni jambo lisilo la kawaida,ujue maisha yangu yote na huu uzee wangu sijawahi kuona kitu kama hiki kinachotokea kwenye huu msiba."
" mzeee kitu gani iko mbona unanitisha.Kuna nini?"
" ni hivi,huu msiba umekuwa ni kama ulishapangwa kuwa utatokea.Maana kila kitu tunachofanya kinakuwa kama ni tayari kilishapangwa.Kwa mfano tumeenda kununua jeneza,tumekuta jeneza limeshaandaliwa likiwa na vipimo ville vile vya sara, pia kuna mtu ambae hafahamiki katuletea mahitaji yote ya msiba."
" mmmmh"
" usigune ndo ivyo,halafu kingine sara aliuwawa saa kumi jioni.Lakini kitu cha ajabu taarifa za msiba wake zilianza kusambaa saa tisa na nusu.Yaani nusu saa kabla hajafa kuna watu walikuwa wanajua sara kafa"
Ndimi
mjamaa samwely kisinga Msendembali -
KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSI YETU - 04
usigune ndo ivyo,halafu kingine sara aliuwawa saa kumi jioni.Lakini kitu cha ajabu taarifa za msiba wake zilianza kusambaa saa tisa na nusu.Yaani nusu saa kabal hajafa kuna watu walikuwa wanajua sara kafa"
Endelea nayo
" mmmmmh! Wewe mzee unauhakika wa ilo?
" ndio nina uhakika.Nusu saa kabla sara hajauwawa nilipigiwa simu kutoka
nyumbani iringa za kunipa pole kuwa sara amekufa.Wakati napigiwa simu tulikuwa wote barazani na sara.Hivyo nikamkatalia aliyenipigia simu nikamuambia ni habari za uzushi.Lakini cha ajabu yeye aliendelea kuniambia yeye ameambiwa kuwa sara kauwawa kwa kuchomwa kisu kifuani."
" mmmmh yeye alijuaje wakati yupo iringa."
" anasema aliambiwa na mtu asiyemfahamu kuwa sara ameuwawa na mumewe"
" mmmh,aya mbona makubwa."
" Ni makubwa sio kidogo,nilipomuuliza kuhusu huyo mtu akasema hamjui ndio
kwanza amemuona siku ile.Na pia aliwaambia waanze maandalizi ya mazishi."
" Yaaani na wewe wakati unaambiwa ayo ,sara alikuwa mzima kabisa?"
" Ndio alikuwa mzima kabisa,tena tulikuwa wote barazani pamoja na mumewe,"
" uliwaambiwa?"
" Hapana sikuwaambia,sikuona umuhimu wa kuwaambia .Kwani baada ya iyo simu hatukukaa sana sara na mumewe wakaenda chumbani kwao"
" duuuh! Aya maelezo uliwaambia polisi?"
" Hapana sikuwaambia,sikuona umuhimu wa wakuwaambia.Pia niliogopa kuwaambia"
" mmmmh! Mzee aya ni makubwa.Kwanza aya maneno nashauri usimwambie mtu mwingine.Tunaweza pata matatizo makubwa sana.Kama kufa sara ameshakufa na mumewe amekubali kuwa ni yeye aliyemuua,hapa hakuna la zaidi,tumzike mwanetu basi ila chonde chonde aya maneno usimwambie mtu mwingine"
"Sawa,wewe ni mtu wa kwanza kukuambia.Sitamuambia yeyote mwingine"
"Kama ni ivyo sawa.Mimi ngoja nikuache basi" aliongea shangazi yake sara na kutaka kuondoka.Lakini kabla hajaenda mbali mzee mkoroma alimwita na kumuuliza.
" halafu ulichoniitia hujaniambia?"
"Daaah! Nilishasahau mzee wangu.Ni hivi kuna marafiki zake sara na wao wanataka kwenda iringa,ila kwakuwa gari nafasi ni chache wamesema watakuja na gari lao.Sasa sijui unasemaje?,niwaruhusu au nifanyeje?"
" mmmh!,waruhusu tu.Kwakuwa wanakuja na gari lao haina shida" alijibu mzee mkoroma,ambae ni babu yake sara.
" halafu baba sara na mama sara sijawaona tangu asubuhi sijui wako wapi?"
" mmmh! Achana nao,Akili zao hazijatulia "
" ok sawa " alijibu shangazi sara na kuelekea walikokaa majirani .
.........................rn
Siku ambayo msiba wa sara ilibidi usafirishwe .John akitembelewa na mama sara pamoja na baba sara.
" pole kwa matatizo mazito john" aliongea mama sara.
" asante ,ila poleni nyinyi pia.Mimi sina tatizo kubwa tatizo kubwa mnalo nyinyi,maana kumpoteza mtoto sio kitu kidogo" aliongea john.
" sio sisi.Wote tuna matatizo .Sisi tumempoteza mtoto lakini wewe umepoteza mke.Lakini ukiachana na kupoteza mke,lakini pia upo gerezani" aliongea baba john.
" daaah! Ndo maisha yalivyo.Lakini kwanini mpo hapa.Mimi ndie ninayeshtakiwa kwakumuua mtoto wenu.Na nimeshakubali kosa kuwa nimemuua,kwanini hamna hasira na mimi? Kwanini hamnishutumu kama wengine wanavyonishutumu?"
" Nakujua vizuri john,na ndio maana nilitaka umuoe mwanangu.Najua upendo wako,najua imani yako.Kamwe hauwezi kumdhuru wala kumuua mtu yeyote" aliongea baba sara,ambae ni baba mkwe wake john.
Maneno ya baba sara yalikuwa ni kama maji kwenye chuma kilichopata moto.Yalimpooza john kweli kweli,alijisikia faraja sana.Watu wote waliokuwa wanakuja kumuona walikuwa wanamshutumu.Lakini wazazi wa sara ndio watu wa kwanza kuamini kuwa yeye hajaua.Alijisikia furaha sana.
" mmmmh! Baba mkwe,unauhakika na unayoongea.Mama yangu mwenyewe anaamini kuwa mimi ndiye niliyemuua
mtoto wenu.inakuwaje nyie wazazi wake mkaamini sio mimi?" aliuliza john.
" Tunaamini sio wewe kwasababu tunakujua vizuri.Sisi ndio tuliokutaka wewe umuoe mtoto wetu.Tulifanya ivyo kwakuwa tulikuona ni kijan mwema,na bado tunaamini kuwa wewe ulikuwa ni mtu sahihi sana"
Maneno yale yalimfanya john atoke machozi.Aliwaangalia wazazi wa sara hakuamini.Taratibu machozi yakawa yanamtiririka mashavuni.
"Lakini john,kwanini umekubali kuwa wewe ndie uliyemuua wakati sio kweli?"
" mmmmh! Mazingira ya tukio yanaonyesha kuwa mimi ndie muuaji.Hata ningekataa vipi isingesaidia.Ningeendelea kukataa bila shaka ningekufa kwa mateso"
" aiseee pole sana.Sisi tumekuja kukutia moyo,na kukuambia kuwa hatuna kinyongo na wewe.Tunaamini wewe hujahusika na kifo cha mtoto wetu.Tunajua kwa mazingira yalivyo ni ngumu kutoka gerezani,ila ishi ukijua sisi hatuna kinyongo na wewe" aliongea mama sara.
" Nashukuru kwa ilo,Mungu hawabariki sana.Maneno yenu yamenipa faraja sana." aliongea john.
" Sara tunamsafirisha leo kwenda iringa kwa mazishi.Ivyo hautamuona tena." aliongea baba sara.
" Natamani ningeenda kumuona lakini najua haiwezekani.Naomba mkaniagie na mimi" aliongea john.
Waliongea mawili matatu kisha wazazi wa sara wakaondoka pale gerezani.Walirudi nyumbani ambapo taratibu zote za safari zilikuwa zimekamilika.
Haikuchukua muda,padre alifika akafanya misa na kuwatakia safari njema.Safari ya kuelekea kijijini kwao ikaanza.Walisafiri wakafika mkoani njombe,ambapo giza lilikuwa limeshaingia.Wakakubaliana wale
chakula cha jioni pale halafu safari iendelee.
Wakiwa wamepaki gari na wanaelekea ndani ya mgahawa kula chakula .Shoga yake sara,aitwae mwajuma alimsogelea shangazi yake sara na kumwambia.
" shangazi subiri kwanza nikuulize kitu?"
" mmmmh! Mwajuma kitu gani icho?"
" ni hivi tangu tunatoka nyumbani kuna gari nimeliona kama linatufatiria,ambalo ni lile pale,halafu saizi nimemuona mtu anayeendesha lile gari.Yule mtu ni kama namjua.Kwenye harusi ya sara alifika,na hata pale nyumbani sara
alipouwawa ni kama nilimuona" aliongea mwajuma.
Ndimi
Mjamaa samwely kisinga Msendembali - songea
KWANINI ULINIUA SIKU YA HARUSi YETU - 05
Tulipoishia - ni hivi tangu tunatoka nyumbani kuna gari nimeliona kama linatufatiria,ambalo ni lile pale,halafu saizi nimemuona mtu anayeendesha lile gari.Yule mtu ni kama namjua.Kwenye harusi ya sara alifika,na hata pale nyumbani sara alipouwawa ni kama nilimuona" aliongea mwajuma.
Endelea nayo.
" mmmh! Mbona ni makubwa aya.Gari lenyewe si lile kule kwenye giza?"
" Ndio ndo lile"
" mmmh mwajuma hili ni jambo kubwa.Ngoja nikamuambie baba sara" aliongea shangazi yake sara huku akielekea walipo mama sara na baba sara.
Mama sara na baba sara walikuwa wameagiza chakula wanakula pamoja.Shangazi yake sara ambaye ni dada wa baba sara alimsogelea baba sara na kumnongoneza sikioni.Baba sara alisimama wakasogea pembeni.
" vipi dada mbona hivi?" aliuliza.
" mmmh kuna shida kaka.Kuna gari linatufatilia toka nyumbani.Halafu mtu mwenyewe anayetufatilia,mwajuma alimuona kwenye harusi,ivyo tunamtilia shaka"
Kabla baba sara hajajibu kitu alimwangalia mkewe kwa macho ambayo yanaonyesha kama kuna kitu kimefahamika ambacho hakipaswi kufahamika.
" mtu mwenyewe yuko wapi ? Aliuliza baba sara.
" Yuko nje kule kwenye gari lake."
" hebu twende," aliongea baba sara na kuongiza njia kutoka nje.
wakiwa wanaelekea shangazi sara alikuwa na wasiwasi sana.Alimshika kaka yake mkono na kutaka kumzuia asiende.
" kaka anaweza kuwa ni mtu hatari.Tunaendaje kienyeji hivi?"
" Punguza uoga.Tanzania ni nchi ya amani.Hebu twende tukamuangalie ni nani?" aliongea baba sara.
Walitembea mpaka pale.Walikuta mlango wa gari umefungwa,na vioo vilikuwa ni tinted,ivyo hawakuweza kuona ndani.Waligonga kioo cha gari .kioo cha gari kikashushwa.
" habari zenu ? " aliongea kijana aliyekuwa ndani ya lile gari. Baba sara baada ya kumuona alionyesha ni kama mtu wanayefahamiana.
" vipi daudi?, na wewe unaenda kwenye msiba wa sara au? " aliuliza baba sara.
" ndio mzee,kwanini nisiende wakati sara alikuwa ni mtu wangu muhimu sana.Lazima niende kumzika na mimi" aliongea yule kijana ,ambae bila shaka jina lake ni daudi kwakuwa baba sara alimwita daudi.
" mmmmh! Kaka unafahamiana naye huyu mtu?" aliuliza shangazi sara.
" ndio namfahamu," alijibu kwa mkato baba sara .
" Tunafahamiana vizuri sana.Vipi mbona gafla tu mmefika kwenye gari langu? Kuna tatizo au?" aliuliza daudi .
"Hapana hakuna tatizo,ngoja tukuache upumzike" aliongea baba sara kisha akageuka kurudi kule walikotokea.Waliingia ndani na kuendelea kupata chakula cha jioni ili waweze kuendelea na safari.
Mwajuma baada ya kuona wamerudi kuongea na yule kijana Alimsogelea shangazi sara na kumuuliza.
" anti vipi? Amewaambiaje yule kijana? Kwanini anatufatilia?" aliuliza maswali mfululizo mwajuma.
"Mmmh! Mwenzangu tumeenda mpaka pale.Lakini kumbe yule mkaka anajuana na baba sara na pia yeye anaenda iringa kwenye mazishi ya sara"
" lakini kwanini alikuwa anatufata kwa siri? Na pia kule kwenye harusi mbona kama alikuwa anahuzuni sana.Nimemuuliza shoga yangu hapa na yeye anasema alikuwa anawasiwasi naye maana kwenye harusi ya sara alimkuta ameinama analia"
" mmmmh ameinama analia? nani huyo?"
" nani vipi? Kwani hapa tunamzungumzia nani? Ni yule kijana.Shoga yangu anet pale anasema kwenye harusi alimkuta kainama analia" aliongea mwajuma.
" mmmmh mwajuma unataka kunichanganya.Hebu tuachane na ayo maana kichwa kitapata joto bure" aliongea shangazi sara.
...........
Kule gerezani John alikuwa mwenye mawazo sana.Alijua mwisho wake umefika.Akiwa amekaa chini akiwaza mengi ,alishituliwa na mfungwa mwenzake aitwae sele.
" mbona unawaza sana ndugu yangu.inabidi uyazoee maisha ya Jela.Mwenzio hapa nina miaka 13 nipo humu ndani,na nimeshazoea.Wewe hata wiki hujamaliza unawaza waza.Uawaza nini?" aliongea sele.
" daaah! Kaka yaaani acha tu. Kilichotokea sijategemea.Ujue kila mtu anaamini kuwa mimi ndiye niliyemuua mke wangu.Lakini leo kwa mara ya kwanza wamefika watu ambao hawaamini"
" mmmh! Wakina nani hao?"
" ni wakwe zangu.Wazazi wa marehemu mke wangu .Wamefika na kuniambia niwe na amani .Wao wanaamini mimi sijaua na siwezi kuua"
" mmmh! Ya ukweli ayo kweli? "
" ndio ni kweli.Nikudanganye hili iweje.Wameniambia wanajua mimi ni mtu mzuri na siwezi kuua"
" aiseeee,yaaani mama yako mzazi hakuamini halafu wakwe zako wanakuamini.Kwa mazingira ya tukio ulivyonieleza ujue hata mimi siamini kama kuna mtu mwingine anayehusika zaidi ya wewe.Yaaani kwa mazingira ya tukio yalivyo ni ngumu sana watu kukuamini."
" kwanini ni ngumu kuniamini.Mimi maisha yangu yote ata kuchinja kuku naogopa,nawezaje kuua mtu,tena kumuua mke wangu mtarajiwa?"
" kwanini isiwezekane.inawezekana vizuri sana.Sasa sikiliza john,kwa maelezo ya tukio yalivyo ni ngumu mtu kuamini wewe hujaua.Kama wazazi wa marehemu wanasema wewe hujaua basi wao watakua wanamjua muuaji?"
" sele acha masihara kwenye mambo makubwa.Wao watamjuaje muuaji?"
" aaah ! Mimi sijui wao watamjuaje,ila swali langu ni kwanini hawaamini wewe ndiye uliyeuwa wakati chumbani mlikuwa wawili tu na mlango ulifungwa?"
Maneno ya sele ,taratibu yakaanza kumuingia akilini john.Akawa anajiuliza moyoni." kwanini wanaamini kwa
asilimia mia moja kuwa mimi sijauwa ? Mmmmh kivyovyote vile watakuwa wanamjua muuaji?" aliwaza john.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza