KWA NINI SIKUSOMA HII!
Uchaguzi wa fani unahusiana sana na kusudi la mtu duniani; uangaliaji wa gifts huathiri sana kuwa na fani sahihi. Kujua kusudi huendana na kujua gifts zako. Kwa Nini Sikusoma hii! Inaunganisha gifts za mtu kutoka kwa Mungu na fani yake.
Miongoni mwa majuto makubwa kwa wahitimu wengi wa vyuo na vyuo vikuu nchini ni Kwa nini Sikusoma fani hii nikaenda fani nyingine
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa karibu asilimia 80 ya watu husoma fani zisizo endana na uwezo wao wa ndani ikijumuisha vipaji na vile wanavyovipenda.
Hatua hii husababisha vijana kuachana na fani zao au kuwa na muda mwingi kufanya wanavyovipenda kuliko walivyosomea.
Pia, uwezo wa kutatua changamoto, ubunifu, tatizo la upatikaji wa ajira na uwezo wa kujiajiri linaendelea kutesa vijana ambao walisoma vitu wasivyovipenda na vilivyo tofauti na uwezo wao wa ndani ikilinganisha na wale waliosoma fani zinazoendana na uwezo wao
Moja ya dalili kubwa kuwa upo katika fani isiyosahihi kwako ni;
1. Huna ujasiri (confidence) kueleza ulichosoma/unachokisoma kwa wengine.
2. Unafanya kwa bidii sana lakini hauridhishwi na matokeo unayoyapata.
3. Malalamiko yaliyokithiri kwenye fani yako.
4. Fani yako haitumiii maarifa uliyo nayo.
5. Unawaza kuacha kila muda n.k
Hakika! Mafanikio katika fani unayoiopenda na inayoendana na gifts Mungu alizokupa ni suala la muda tu!
Leo, nimekuletea e-book yangu inayoitwa Kwa Nini Sikusoma Hii! ambayo utajifunza namna sahihi ya uchaguzi wa fani ikihusisianisha uwezo wako wa ndani (Core Genius)
Karibu kusoma kitabu hiki, hutabaki ulivyo.