AKILI ILIYO SAHIHI:
Ina uwezo wa kufumbua matatizo yake. Akili inayohitajika, lazima iwe na uwezo wa kutatua au kufumbua
matatizo yake. Kazi ya akili ni kutoa ufumbuzi wa matatizo, au kutoa msaada wa jinsi ya kufanya au kufanikisha
jambo fulani. Akili timamu, linapotokea tatizo, hutoa
njia ya kulitatua.
Lengo tujue kuwa, sio kila akili inafaa, au sio kila akili ni
nzuri. Yafaa tujue kuwa kuna aina nyingi za akili, lakini
tunachokitafuta kujua akili zilizo bora zaidi ya nyingine.
Hakuna maana ya kuwa na akili ambayo ukiwa
na tatizo inashindwa kutoa ufumbuzi. Kama una
kalikuleta(kikokotoo) lakini unapoipa hesabu haitoi majibu au inachanganyikiwa je kuna maana gani ya kuwa
na kalikuleta kama hiyo? Ninacho maanisha hapa ni kukujulisha kuwa, ubora wa akili ni kazi zake inazofanya
au iwapo zitamsaidia aliye nazo kufumbulia matatizo
yake magumu. akili ni “problems solver:
Kwa hiyo basi, inafaa tuupime ubora wa akili katika
uwezo wake wa kutoa ufumbuzi kwa mwenye nazo.
Neno akili tunaweza kuliita jina lingine nalo ni “Utambuzi” Utambuzi, ni hali ya kugundua au kujua baada ya
kutokujua, au kufichua kile kilicho fichika. Akili lazima
iweze kutambua vitu ambavyo kwa kawaida ni vigumu
kuvijua au kuvipatia utatuzi
"KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI"
Ni kitabu maalumu kwako, msomaji wangu, ili kikusaidie katika kukupatia mbinu bora za kukuwezesha kuwa na uwezo mkubwa kiakili(Kuongeza akili na kuzitibu akili, na kuzitumia kwa manufaa). Kitabu kitakusidia kujua nini maana ya akili, na jinsi ya kuziongezea uwezo (Au kuzitunza), na pia jinsi ya kuzitumia vizuri,
Zikuletee matokeo chanya katika maisha yako.
Wazo la kukuandikia kitabu.
Wazo la kukuandikia kitabu hiki limetokana na kitabu
nilichoandika, kiitwacho KUWATUNZA WAZEE NA
VIKONGWE. Baada ya kufanya tafiti za matatizo ya
mabadiliko ya maumbile ya wazee haswa ya kiakili,
ndio kimekuwa chanzo cha kupata wazo hili la kuaandika kitabu maalumu cha kuongeza uwezo wa kiakili.
Nilipokuwa nafanya tafiti zangu nimegundua kuwa watu wengi wanahitaji msaada mkubwa wa kujua jinsi wanavyoweza kuzihudumia akili zao au kuzitunza au kuzisaidia ili ziweze kuleta matokeo makubwa katika maisha yao.
Watu wengi hawajajua umuhimu wa kuzitunza akili zao, aidha hawajui jinsi ya kuzisaidia akili zao ili ziweze kuwa na matokeo ya hali ya juu. Aidha tukija katika masuala ya elimu(wanafunzi), tunaona wanafunzi wengi wanashindwa kufaulu vizuri darasani, lakini chanzo kikubwa ni kushindwa kujua kanuni za kuzifanya akili zao ziwe na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.
Wanafunzi wengi wanashindwa kufaulu kwa sababu ya udhaifu wa akili, au uwezo mdogo wa akili katika kufikiri na kupambanua mambo. Aidha wanafunzi wengi wanakumbwa na matatizo ya kusahau au kutokuzingatia pale wanapofundishwa darasani, hii ni moja ya shida ya udhaifu wa akili
Katika tafiti zangu kadha nimegundua kuwa, kati ya watu 100, wenye uwezo mzuri wa kufikiri wanaweza kuwa asilimia 5% tu. Asilimia nyingine hawana uwezo mzuri wa kufikiri kwa sababu ya udhaifu wa akili zao. Ninaposema udhaifu wa akili sina maana kutokuwa na akili kabisa, hapana. Bali akili zao zimekosa uwezo wa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. Mfano: Iwapo gari injini yake ikiwa na shida inaweza isiwe na ufanisi au hata mwendo wake unaweza kuwa wa pole pole, kwa sababu injini inatatizo. Hali kadhalika iwapo mtu ubongo wake unashida, au umekosa mahitaji yake muhimu ya kuuwezesha ufanyekazi zake sawasawa, nao hautafanya kazi ipasavyo.