Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kuuweza Wakati Ujao - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

KUUWEZA WAKATI UJAO

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 28, 2024
Product Views:
30
In category:
Sample

Kila mmoja wetu anayo matamanio ya kuwa mtu fulani hapo baadae na kila mmoja wetu ana malengo, ndoto na maono ambayo anatamani yatimie siku za usoni. Sasa ili kuweza kuyatimiza matamanio yote ambayo unayo ni lazima ujiandae kimwili, kiroho na kiakili kuweza kuwa mshindi katika hayo. Ukiona mtu yeyote anakuwa mshindi katika majira aliyokuwepo ujue kabisa haikutokea kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya maandalizi ya kutosha aliyoyachukua kabla majira hayo ya ushindi hayajafika. kitabu hiki ni kitabu ambacho kitakufunulia siri na kanuni ambazo zitakusaidia kujiandaa kuwa mshindi katika nyakati zote na katika kila eneo la maisha yako ikiwemo; ndoa, utumishi, biashara, karama na vipaji vyako, uongozi, elimu nk.Ninaamini kabisa watu wote waliokuwa washindi leo hii waliandaliwa na walijiandaa kuwa washindi hivyo na wewe unayetaka kuwa mshindi kitabu hiki nilichokiandika kitakuandaa na kukupa mbinu za kukufanya kuwa mshindi sasa na nyakati zijazo.

Moja ya mbinu kubwa ambayo iliyasaidia majeshi mengi duniani kushinda vita zao ni kuwatuma baadhi ya watu kwa siri ili kwenda kupeleleza katika nchi ya adui na kujua wao wamejipanga vipi kupigana vita yao ili wao watafute na waende na mbinu bora zaidi ili wawashinde katika uwanja wa vita.

Kwa maana nyingine walitamani kujua adui zao walipanga nini na wamejiandaa vipi kupigana vita yao wakati wa vita unapokuja.

Yoshua 2:1

“Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.”

Wakati nilivyokuwa naendelea kutafakari Mungu akanifunulia siri kubwa sana juu ya majira na nyakati. Akanifundisha kuwa; maisha yetu hapa duniani sisi tuliokoka ni kama wanajeshi ambao tupo vitani na vita hii itaisha siku ambayo Yesu atarudi na kuwachukua watu wake. Akanifundisha tena ya kuwa; ili watu wa Mungu waweze kushinda katika kila eneo la maisha yao ni lazima wajifunze namna ya kuuweza na kuumiliki wakati ujao.

Mungu akanionyesha namna ambavyo watu wa ufalme wa giza wanakesha usiku na mchana ili kukamilisha ajenda zao na mipango yao ya wakati ujao.

Kuna mambo mabaya leo hii yanatokea katika uso wa nchi lakini ni mambo ambayo yalipangwa na kuandaliwa miaka ya nyuma kabla hata ya wakati huo haujafika na kabla hata ya hayo mambo hayajatokea.

Hii ikanionyesha ya kuwa; inawezekana kabisa sisi leo hii tukajiandaa na kujipanga kuitawala na kuimiliki kesho zetu kabla shetani hajaiba au kuharibu kesho zetu.

Lengo kuu la kuandika kitabu hiki.

Kitabu hiki nimekiandika nikiwa na malengo makuu matatu;

  • Kuwaandaa watu wa Mungu kiroho, kimwili na kiakili kuukabili wakati ujao.

Kuwa na ushindi na mafanikio kwa wakati unaokuja unahitaji wewe binafsi kuwa na maandalizi ya kutosha ili kukuwezesha na kukusaidia kushinda.

Usipokuwa na maandalizi ya kutosha maana yake wewe utashindwa vita. Watu wote ambao wanashindwa vita zao kwa namna moja au nyingine walikosa kuwa na maandalizi mazuri juu ya kesho zao.

Maandalizi yako ya kutosha ndio ambayo yatakupa ujasiri wa kuwa na kesho iliyo bora.

Ni kweli tunahitaji kuwa na imani kubwa katika kuuweza wakati ujao lakini Neno la Mungu linasema kuwa imani bila matendo imekufa kwa maana yake ili imani yako ya ushindi juu ya wakati unaokuja ifanye kazi lazima ufanye matendo ambayo yatakuandaa na yatakusogeza karibu na ushindi wako.

Tunajiandaa sio kwa sababu tunajua kesho yetu itakuwaje ila tunajiandaa kwa sababu hatujui nini tunahitajika kuwa nacho nyakati zijazo.

Unamkumbuka Daudi?

Daudi alivyokuwa anachunga kondoo za baba yake, alikuwa akipigana na simba na dubu waliokuwa wanajaribu kula kondoo bila ya yeye kujua kuwa hayo yalikuwa ni maandalizi kwa ajili ya kupigana na Goliati.

Vipi kama angeamua tu kukimbia akaacha kondoo waliwe?

Kwahiyo,hiki kitabu nimekiandika kwa ajili ya kumuandaa mtoto wa Mungu kuikabili kesho bila ya kuwa na hofu au mashaka ya mambo yanayoendelea duniani bali kuwafanya kesho zao kuwa kesho zenye ushindi na mafanikio makubwa.

  • Kuwaonyesha watu wa Mungu njia na mbinu ambazo zitawasaidia kuweza na kushinda wakati ujao.

Nimeandika kitabu hiki pia ili kuwasaidia watoto wa Mungu kwa kuwapa mbinu, njia na siri ambazo kama wakizitumia wataweza kuushinda wakati ujao.

Wewe kama mtoto wa Mungu upo katika vita kali sana katika ulimwengu wa Roho na kazi kubwa ya adui ni kuhakikisha kuwa anakupoteza au anakupeleka katika njia za upotevuni ili wewe usiweze kufikia kesho yako iliyo bora.

Kwahiyo wakati shetani anapambana kuandaa mipango kwa ajili ya kuharibu ndoa yako, biashara yako, huduma yako na maisha yako ya baadae wewe pia unatakiwa kupambana kuhakikisha unavaa silaha za vita za Kimungu na kutumia siri na njia zilizomo katika kitabu hiki ili uweze kushinda.

  • Kuwapa watoto wa Mungu akili za kujua mambo yanayowapasa kuyafanya kwa wakati huu na ule unaokuja. 

Neno la Mungu linasema katika kitabu cha;

1 Nyakati 12:32

“Na wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.”

Ili kuuweza wakati ujao ni lazima watoto wa Mungu wawezeshwe kwa kupewa akili ya kiungu ambayo itawawezesha kujua ni mambo gani wanayotakiwa kuyafanya kwa majira waliopo au kwa majira yanayokuja.Usipojua nini inakupasa kufanya ni rahisi sana wewe kushindwa na mazingira na hali zozote za wakati unaokuja, hivyo hiki kitabu kitakuwezesha wewe na kuitia akili yako nuru ili ujue yote yanayokupasa kutenda kwa majira na nyakati husika.

Ninaamini baada ya kumaliza kusoma kitabu hiki utakuwa umejazwa na hekima na ufahamu wa kutosha wa ni kwa namna gani utaweza kuuweza na kushinda wakati unaokuja.

Mungu akubariki sana na karibu kusoma kitabu hiki….

More Products On Discount
5,000 Tsh. 2,500 Tsh.

Sold by: Joyce Mwakajonga

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

25,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Msafiri Lwihula

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
Old is Gold