KUUNGANISHWA MIFUKO YA PENSHENI, JE MAFAO YAMEKUWA BORA?
Mwaka 2018 serikali ilifanya uamuzi wa kuunganisha Mifuko ya Pensheni yaani LAPF, PSPF, GEPF na PPF kuunda Mfuko mpya wenye jina la PSSSF yaani Public Service Social Security Fund. Swali la kujiuliza, Je serikali ilifanya hivyo ili kuboresha mafao ya wafanyakazi wanaochangia Mifuko hiyo? Swali hilo limejibiwa kwenye Kitabu hiki.
Ndani ya Kitabu hiki utajifunza Masuala yoye yahusuyo Mifuko ya Pensheni nchini, Historia ya Hifadhi ya Jamii Tanzania kabla na baada ya Uhuru mwaka 1961. Utafahamu historia ya kila Mfuko yaani LAPF, GEPF, PPF, PSPF, NSSF na ZSSF. Utafahamu na chimbuko la kuanzishwa kwa PSSSF mwaka 2018 na hatma ya mafao ya wafanyakazi kwa miaka ijayo.
Kitabu kinafafanua changamoto za kuunganisha Mifuko yote na kubakiwa na Mifuko miwili tu yaani PSSSF na NSSF. Changamoto za kuondoa ushindani kwenye sekta hii zimedadavuliwa.
Mbinu za kuongeza wananchi zaidi ya milioni 10 kwenye Mifuko hii miwili zimefafanuliwa.
Watu wote wanaotaka kujua Hifadhi ya Jamii na jinsi ya kuimarisha sekta hii, kitabu hiki kitawafaa sana. Wanasiasa, watunga sera, wasomi na wachambuzi wa sera kitabu hiki kinawafaa sana.
USIKOSE KITABU HIKI KWA ELIMU PANA ZAIDI YA HIFADHI YA JAMII.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza