Kutawala Vifaa Vyako Vya Muziki: Kanuni Za Msingi
Kutawala Vifaa Vyako vya Muziki: Kanuni za Msingirn[ Mastering Your Music Gear: The Basic Principles ]
Kitabu hiki kitakufanya ujue kuwa sio kila sauti kubwa ya muziki ina usikivu himilivu (intelligible). Maeneo mengi sana kwenye nyumba za ibada, kumbi za harusi na matamasha huwa hawana shida na ukubwa wa sauti (Loudness). Hata hivyo, unapokaa kusikiliza nyimbo au kinachoongelewa kupitia vyombo hivyo vya muziki inakuwia vigumu sana kuelewa nini kimezungumzwa. Unapojifunza mbinu hizi za jinsi ya kuvitumia vyombo vya muziki itakufanya uongeze usikivu kwenye vyombo vya muziki.
Utajifunza kwenye kitabu hiki kuwa, sauti kubwa kupita kiasi ni hatari kwa afya ya binadamu na wengi wao hawafahamu hili.
Kitabu hiki kimetoa mwongozo wa kiwango cha sauti (volume) kinachopaswa kutumika katika vyombo vyako. Wapo baadhi ya watu wanafurahia kuwa karibu sana na spika linalotoa sauti kubwa bila kujua matatizo ya kiafya wanayoweza kuwapata kutokana na sauti kubwa kupita kiasi.
Kwenye kitabu hiki nimetoa ushauri wa vifaa gani utumie kupima ukubwa wako wa sauti ili uweze kudhibiti sauti yako isiweze kuleta madhara kwa wasikilizaji.
Benson E. Msechu
Mwandishi wa Kitabu