KUTAFUTA UPAKO MARADUFU
Upako ni nguvu za Mungu za utendaji zinazotuwezesha kupata matokeo makubwa katika eneo fulani.Maandalizi ya kiroho ni ya muhimu katika Kutafuta upako zaidi wa huduma.Safari ya kutafuta upako Zaidi, itakugharimu kufika maeneo ya kiroho na viwango vya kiroho, ambavyo hujawahi kuvifika katika maisha yako yote.Kupokea upako maradufu ni kitu kigumu, kwasababu hiyo ni watu wengi wanaojaribu na wachache wanaofanikiwa. Kuna masharti na maandalizi yanayohusika katika upako wa huduma. Mungu anatutaka tutake sana na kuwa na shauku na upako ambao hatunao kwasababu upako ndio kitendea kazi cha muhimu kabisa katika huduma. Bila ya upako, maarifa yako yote ya chuo cha Biblia na vyeti vyako vyote ni bure. Unahitaji upako na upako hauji kwa kwenda shule ya Biblia, Upako haufundishwi, upako unatafutwa na kukamatwa.
KUTAFUTA UPAKO MARADUFU NI KITABU KIZURI SANA NA KINAMFAA KILA MTU AMBAYE YUPO KATIKA HUDUMA AKIMTUMIKIA MUNGU. KIMEFUNDISHA KWA KINA SANA NAMNA AMBAVYO MTUMISHI ANAWEZA KUUTAFUTA UPAKO NA KUKONGEZA UTENDAJI WA UPAKO KATIKA UTUMISHI WAKE.