KUSUDIA KUWA WEWE
ONESHA UNACHOWEZA KUFANYA KULIKO MAPUNGUFU YAKO
Mungu alimuumba mtu kwa kusudi maalum. Hili ndilo jambo ambalo linalomfanya mtu anakuwa na shauku au msukumo wa ndani wa kufanya jambo fulani hata kama wengine wanaona tofauti au haliwezi kufanyika. Mungu hakuishia kuweka kusudi na kutufanya kusikia shauku toka ndani kiasi cha kuanza kufanya mambo la! hasha aliweka uwezo wa kufanya jambo husika ndani ya mtu ambao hauonekani kwa macho ila hudhihirika pale mtu anapochukua hatua ya kuanza kufanya jambo fulani. Sote tuliumbwa na Mungu lakini hatukuitiwa kusudi la namna moja na wala hatukupewa uwezo sawa, hapa namaanisha tumetofautiana uwezo wa kufanya mambo kulingana na kila mtu anachofanya. Hakuna mwanadamu anayeweza kutambua kusudi la mwenzake wala kuona kwa macho mwenzake alipewa nini ama sivyo mtu mwenyewe ameonyesha ustadi wake katika kufanya jambo fulani. Katika mchakato mzima wa mtu kuonyesha kile anachoweza kufanya huwa kuna asilimia ambazo zinaonyesha jinsi asivyoweza kwa maana ya yale yanayopungua kwake. Kwa kifupi mapungufu ni mambo ambayo mtu anayakosa. Hivyo basi ili mtu aweze kufanya vizuri zaidi anahitaji kutilia mkazo zaidi katika uwezo wake na si mapungufu yake. Kitabu hiki kimeandaliwa mahususi kukukumbusha na kukutia moyo ili ujikite katika kuwekeza zaidi kwenye kile unachoweza kufanya kuliko mapungufu yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza