Kusanya Vipande Vyake
Kila jukumu unalo lipata yakupasa ulifanye kwa ukamilifu.
Kusanya Vipande Vyake ni hadithi inayo muhusu binti aitwaye Furaha. Binti ambaye amekutana na changamoto nyingi mno na nzito za kimaisha Hadi kumpelekea kua ni binti mkorofi sana, jeuri, kisirani, anaye mchukia kila mtu na hadi kujichukia yeye mwenyewe. Kijana mnyenyekevu, mpole, msomi, na tajiri, anapewa jukumu zito la kumtafuta binti huyo (ambaye hawafahamiani kabisa) ili aweze kukusanya vipande vyake, haikua kazi nyepesi lakini anaamrishwa aifanye.
Je, kijana ataweza kweli kulitimiza jukumu alilopewa? Na je, wajua ni vipande vya aina gani anapaswa kumkusanyia huyo binti?
Fuatilia kwa undani zaidi katika kitabu hiki ambacho hakika mbali na kukuliwaza, kitakufundisha mambo mengi.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza