
KURUDI KWA YESU NA DALILI ZAKE KUU
KURUDI KWA YESU NA DALILI ZAKE KUU
DIBAJI
Biblia ina masomo mengi sana, mengine yanajulikana kama masomo mepesi kwa sababu yako wazi kwa kila mtu kama vile:nimani, upendo, neema, wokovu, ushindi juu ya dhambi, utumishi, na mengine mengi. Lakini yapo pia masomo yanayojulikana kuwa masomo magumu; si kwa sababu hayafundishiki, bali kwasababu yana mitazamo ya waalimu iliyo tofauti tofauti kiasi kwamba, hata wasikilizaji wanachanganyikiwa wanapoyasikia, nayo ni kama vile: Kuja kwa Yesu mara ya pili, dhiki kuu,utawala wa Yesu wa miaka elfu duniani, kuumbwa kwa mbingu mpya na nchi mpya, karamu ya Mwana-kondoo, na kufungwa kwa Shetani.
Biblia ni kama somo la hisabati ambazo, usipozijua kanuni zake, huwezi kupata jibu sahihi kamwe; utakuwa mtu wa kukosea kila siku. Katika kitabu hiki, nimejitahidi kufundisha somo la kurudi kwa Yesu mara ya pili, ambalo ni somo muhimu kwa kila mkristo aliye na tumaini la Bwana Yesu. Nimetumia kanuni muhimu za kusoma na kuifasiri Biblia, ili kukupatia fasiri iliyo sahihi, na isiyo na maswali. Namshukuru Mungu kwamba, tukisoma Biblia bila kufuata itikadi za kidini, ni kitabu kinachoelewekanvizuri sana.
Nakutakia neema ya Bwana Yesu Kristo iwe juu yako, unapojifunza kwa kukisoma kitabu hiki.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza