Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kuja Kwa Yesu Mara Ya Pili - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

KUJA KWA YESU MARA YA PILI

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 16, 2025
Product Views:
67
In category:
Sample

KUJA KWA YESU MARA YA PILI:- Mwl. Iman Kamwela

Kama tunakutarajia kuja kwa Yesu mara ya pili, bila shaka tunamaanisha kuna ujio wake wa kwanza uliowahi kukamilika. Kila safari imebeba sura ya kipekee japokuwa hii ya pili haijatimia lakini kwa msaada wa maandiko tunaweza kujua itakuwaje na hivyo kuwa rahisi kwetu kutofautisha.

Ujio wa kwanza ulikuwa wa kinyonge sana maana katika huo alidharauliwa, alitukanwa na hatimae kuuawa na watu waliokuwa kinyume nae. Haya yalifanikiwa kwa sababu alivaa sura ya mwanakondoo iliyomlazimu kuwa tayari kuvumilia mengi mabaya ili alitimize lengo (kusudi) lililomleta duniani, nalo si lingine bali kuleta ukombozi kwa mwanadamu dhidi ya dhambi iliyokuwa inamtesa na kumtenganisha na uso wa Mungu. Kwa kupigwa kwake mimi na wewe tumepona, mateso tuliyostahili aliyagongomelea
msalabani.

Kuja kwa Yesu mara ya pili ni tukio nyeti linaloenda sambamba na matukio mengine ya wakati huo. Baadhi ya matukio yanayohusiana na kuja kwa Yesu mara ya pili ni pamoja na unyakuo, arusi ya mwanakondoo, dhiki kuu na utawala wa Yesu duniani miaka elfu moja.

Miongoni mwa wahusika wakuu katika matukio hayo ni Yesu, kwani katika hayo yote yapo yatakayotokea kabla hajashuka na mengine baada ya kushuka. Yatakayotokea kabla hajashuka kwa namna moja ama nyingine tunaweza kusema yatakuwepo maalumu kwa ajili ya kuandaa mazingira ya Yesu kurudi duniani na yale yatakayotokea baada ya kuja kwake duniani ndiyo yatakayohitimisha kusudi lake la kuwepo duniani kwa mara nyingine.

Bila shaka ndani ya kitabu hiki utaelewa kwa mapana sana kwa habari ya uhusiano unaonenwa katika paragrafu hii. Kwa jinsi hiyo kipaumbele kikubwa ndani ya kitabu hiki ni kuchanganua matukio yanayoujenga (yanayo uandalia mazingira) ujio wa Yesu mara ya pili lakini vilevile ni nini kitafanyika baada ya ujio huo.

Ndugu msomaji wangu ninakusihi katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, ukiwa katika mchakato mzima wa kuendelea kuusoma na kuutafakari ujumbe unaopatikana katika kitabu hiki, hitaji na omba sana juu ya uongozi na msaada wa Roho Mtakatifu. Maana kwa kufanya hivyo unaweza kujifunza na kupata ujumbe yamkini zaidi ya hata huu ulioandikwa ndani ya kitabu hiki. Hii ni kwa sababu mtafsiri mkuu wa mafumbo ya Mungu ni Roho wake (Roho Mtakatifu) na huyo ndiye ajuaye kipimo cha njaa uliyonayo kwa jinsi ya rohoni, hivyo anaweza kukuandalia na kukupatia chakula kinachoweza kukutosheleza na kukufaa ili upate kukila na kushiba. Ubarikiwe sana na karibu.
More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold