KUISHI KAMA TAI
Tai ni alama na picha ya ushujaa, ujasiri, kuwa na maono na kuwa mpambanaji. Ni alama ya mtu mwenye nguvu na maisha ya ushindi. Tai anaheshimika na kusifika kwa fikra zake na mtazamo wake, unaomtofautisha na ndege wengine wote na kumfanya kuwa ni Mfalme wa Anga. Mambo makuu tunayojifunza kutoka kwa tai ni pamoja na uwezo wake wa kuona mbali, kukabili dhoruba, kulenga jambo, kuyakabili mabadiliko, kufanya mahusiano, kujihuisha upya mwenyewe na nidhamu yake binafsi. Kila mtu anaweza kuwa tofauti na alivyo sasa. Kama tai, na sisi tunaweza kujitofautisha na watu wengine na kuwa watu wa kipekee. Ikiwa unataka kuwa mtu wa tofauti basi kitabu hiki kitakusaidia kukupa hamasa ya kubadilisha fikra zako na kwa kuzifuata kanauni za maisha ya tai unaweza kuwa mtu mkuu na wa kipekee
KUISHI KAMA TAI NI KITABU CHA KUMOTISHA NA HAMASA YA KUWA NA MAISHA YA USHINDI NA MAFANIKO KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA. KANUNI SABA ZA MAISHA YA TAI ZIMEFUNDISHWA AMBAZO UKIZITUMIA NA KUZITEKELEZA KATIKA MAISHA YAKO, BASI NAWE UTAKUWA NA MTAZAMO WA TAI.