KUFUNGULIWA TOKA KATIKA VIFUNGO NA MAGEREZA YA IBILISI
Huduma ya Maombezi ilikuwa ni kiu kubwa iliyokuwa moyoni mwangu kwa muda wa miaka mingi sana, Kitabu hiki ni matokeo ya harakati zangu za kumtafuta Mungu ili anitumie kufungua watu wake
Kwa muda mrefu nilifanya maombezi lakini matunda yake yalikuwa madogo sana, nilikutana na wagonjwa wengi nikawaombea; wengi wao hawakupokea; hali hii ilinikatisha tamaa sana. Nakumbuka mkutano nilioufanya mwaka 2013, nilikutana na watu wengi waliofungwa na wakaletwa katika eneo la mkutano; nilijaribu kufanya huduma hiyo ya maombezi; wengi wao hawakufunguliwa. Ndipo nilipoamua tukiwa na rafiki yangu kuelekea mlimani kwa ajili ya maombi; kwa nadhiri ya kwamba, mpaka Bwana aseme neno
ndipo tutakaposhuka mlimani.
Ile tunaianza siku ile ya tatu tukiwa tumechoka na tumelowana sana kwa sababu ya mvua zilizokuwa zikinyesha; mchana ule nikasikia amani ya kutoka katika maombi yale. Basi tukashuka katika mlima ule, tulikuwa katika kijiji kimoja kinaitwa Ng’obho kilichopo katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Tulipotoka kwenye maombi, tukafika kwa mama mmoja akatupokea na kutuandalia chakula. Usiku ulipoingia tukaenda kupumzika nikiwa nimechoka kabisa; ndipo kuanzia saa mbili za usiku wa tarehe 27/04/2013, nikafunuliwa masomo yaliyozaa kitabu hiki. Sauti ikaanza kusema nami ile naingia tu kitandani, wala haikuniacha kupata usingizi mpaka saa kumi na mbili za asubuhi ndipo mafunuo hayo yalipokoma. Maombi yangu ni kwamba; kazi hii ya uandishi ikuinue katika huduma yako, ukatoke katika vifungo alivyokufunga adui, hatimae uwe huru kabisa “Mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru” Yohana 8:32.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza