KUANGUKA KWA KIONGOZI
Kuna hatari nyingi zisizoonekana katika uongozi. Kadiri unavyokuwa katika utumishi na uongozi wa kiroho kwa muda mrefu, ndivyo utavyotambua vile ulivyo wazi na karibu zaidi na kuanguka. Kadiri unavyotambua kwamba ni neema tu ya Mungu ndio inaweza kukutunza, kukuhifadhi na kukufanya ubaki mwaminifu na hatimaye umalize vema, ndivyo unavyokuwa salama zaidi. Moja ya makosa ya kawaida wanayoyafanya watumishi wengi ni kujiamini kupita kiasi na kuona kwamba wapo salama. Haijalishi wewe umekuwa mtumishi na kiongozi kwa muda gani, na kwa kiwango gani, hatari na mitego ipo ina kusubiri. Kadiri mtumishi na kiongozi anavyokwenda juu sana ndivyo hatari zinavyoongezeka.
KUANGUKA KWA MTUMISHI : HIKI NI KITABU CHA LAZIMA KWA KILA MTUMISHI. KIMEFUNDISHA HATARI NA MITEGO UILIYOPO KATIKA UTUMISHI AMBAYO KILA MTUMISHI HANA BUDI KUJILINDA NAYO.