KIONGOZI MTUMISHI
Suala la uongozi wa kiutumishi ndiyo tofauti kubwa zaidi iliyopo kati ya uongozi wa kiroho na wa kiulimwengu. Katika kipindi chake cha huduma cha miaka mitatu na nusu, Yesu alidumu kuwafundisha wanafunzi wake kwamba uongozi ulimaanisha utumishi, kinyume na “hali ya kuwa juu ya wengine” ambayo watu wa mataifa waliionesha siku zile (Mathayo 20:25)
Kuna maelfu ya vitabu vimeandikwa kuhusu uongozi, lakini vichache kuhusu utumishi. Nimeandika Kitabu hiki mahususi ilikutoa changamoto kwa viongozi wa leo kurudi kwenye falsa ya Yesu kuhusu utumishi. Kitabu hiki kime sheheni mafundisho mazuri ya juu ya Uongozi wa kiutumishi ambayo ni matokeo ya mafundisho mengi niliyojifunza toka kwa waalimu wengine wa Uongozi na yale ambayo nimeyafundisha katika semina na makongamano mbalimbali ya uongozi.
Ni hakika baada ya kukisoma mtazamo wako juu ya uongozi na utumishi utabadilika.
Mungu akubariki .