KIKOKOTOO
KIKOKOTOO DAVID NGOCHO SAMSON MUHTASARI Maisha duni ndiyo yalimpa motisha wa kupambana na umaskini na kuushinda. Akatia bidii kwenye masomo, akafaulu kila hatua. Enzi zile, elimu ilikuwa bure hadi vyuo vikuu, chini ya serikali ya awamu ya kwanza ikiongozwa na hayati mwl JK Nyerere. Mtaji pekee ilikuwa juhudi binafsi kwenye masomo. Alipofanikiwa kuondokana na ufukara, Muganyizi hakupenda masahibu aliyopata yeye, yampate mwanaye, akawekeza kwenye elimu ya wanae na kuyaboresha maisha yao. Wakafanikiwa kupata kazi zenye marupurupu na mishahara minono, isipokuwa kitinda mimba, Mutahaba. Muta alizaliwa kwenye ukwasi, hakupata fursa ya kukabili changamoto zake, hizo zilishughulikiwa na baba pamoja na kaka zake matajiri. Hali hiyo ikamlemaza, hata hakujua nini cha kufanya pale umaskini ulipobisha hodi kwenye familia yao. Ni Baada ya kaka zake kusemekana kufa kwa kunyongwa huko ughaibuni kwa kosa la kujihusisha na Biashara ya dawa za kulevya, huku baba yake, Mzee Muganyizi akidhulumiwa fedha za pension ya kustaafu na kundi la kihalifu la watu wenye pesa, wenye nguvu za kuficha baadhi ya watumishi na Viongozi wa serikali mifukoni mwao, Muta analazimika kujifunza maisha kwa mbinde na kwa kukabili hatari. Riwaya hii itakupitisha kwenye harakati za hatari anazopitia Muta ili kuyasimamisha maisha yake kwenye mstari autakao. Kwake, umaskini haukubaliki.
KIKOKOTOO
DAVID NGOCHO SAMSON
MUHTASARI
Maisha duni ndiyo yalimpa motisha wa kupambana na umaskini na kuushinda. Akatia bidii kwenye masomo, akafaulu kila hatua.
Enzi zile, elimu ilikuwa bure hadi vyuo vikuu, chini ya serikali ya awamu ya kwanza ikiongozwa na hayati mwl JK Nyerere. Mtaji pekee ilikuwa juhudi binafsi kwenye masomo.
Alipofanikiwa kuondokana na ufukara, Muganyizi hakupenda masahibu aliyopata yeye, yampate mwanaye, akawekeza kwenye elimu ya wanae na kuyaboresha maisha yao. Wakafanikiwa kupata kazi zenye marupurupu na mishahara minono, isipokuwa kitinda mimba, Mutahaba.
Muta alizaliwa kwenye ukwasi, hakupata fursa ya kukabili changamoto zake, hizo zilishughulikiwa na baba pamoja na kaka zake matajiri. Hali hiyo ikamlemaza, hata hakujua nini cha kufanya pale umaskini ulipobisha hodi kwenye familia yao.
Ni Baada ya kaka zake kusemekana kufa kwa kunyongwa huko ughaibuni kwa kosa la kujihusisha na Biashara ya dawa za kulevya, huku baba yake, Mzee Muganyizi akidhulumiwa fedha za pension ya kustaafu na kundi la kihalifu la watu wenye pesa, wenye nguvu za kuficha baadhi ya watumishi na Viongozi wa serikali mifukoni mwao, Muta analazimika kujifunza maisha kwa mbinde na kwa kukabili hatari.
Riwaya hii itakupitisha kwenye harakati za hatari anazopitia Muta ili kuyasimamisha maisha yake kwenye mstari autakao. Kwake, umaskini haukubaliki.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza