
Kijiji Kisicho Na Makaburi
Kijiji Kisicho na Makaburi
“Hakuna ubishi, simulizi iliyobeba riwaya hii inaakisi falsafa ya Kiafrika kwa kina na mapana. Ama pia niseme inaonesha mivutano ya kani za dini za kigeni na mpinzani wake mkuu “tamaduni za Kiafrika” ambaye ameoneshwa kihasi. Riwaya imebeba dhana pana zaidi. Tofauti kubwa ya Dickson Mtalaze na waandishi wengine wa simulizi za kutisha ni uwezo wake wa hali ya juu wa kuyaeleza matukio ya kuogopesha lakini kwa namna ya kifutuhi. Siwezi kuacha kusema kuwa, tangu naanza kusoma riwaya yake, hakuacha kunivunja mbavu na papo hapo kunitisha. Huu ni ufundi wa kipekee!”
Gervas Kasiga
Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dodoma
“Nimesoma riwaya nyingi zilizoandikwa na watunzi wa Kitanzania lakini hii ina uzuri na upekee. Inagusa moyo na fahamu na kumuacha msomaji atamani hadithi isiishe. Hongera Mtalaze.”
Prof. John P. Mwakyusa
Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza