KANISA NA TEKNOLOJIA
Kitabu hiki kinaonesha kuwa kwa wakati wetu mbinu za kuwasilisha ujumbe zimebadilika kabisa ukilinganisha na za Yesu, Paulo na mitume wengine. Leo hii watu wanawasiliana kwa teknolojia ya habari zikiwemo barua pepe (email), facebook, WhatSapp, Youtube, na zingine nyingi. Dunia imehamia huko na kanisa linapaswa kuhamia katika ulimwengu
Yesu hajataja mbinu ambazo
tutazitumia wakati wote kwa vizazi vyote. Yeye alizunguka huko na huko
akihubiri hadharani na manyumbani, katika maziwa na visima katika nchi ya
Palestina. Paulo akatumia mbinu ya kusafiri na kuvuka mipaka ya kimataifa hadi
Asia ndogo akikutana na watu mbalimbali wakiwemo wafalme na wasomi kwenye
maeneo ya kumbi, masinagogi, viwanja vya riadha vya kiyunani na akaongeza mbinu
mpya ya kuwasilisha ujumbe kwa barua (nyaraka za Agano Jipya). Kwa mifano hiyo
ya Yesu na Paulo tunaweza kusema kwa usahihi kabisa kuwa mbinu za kutekeleza
agizo kuu zinabadilika kutoka kizazi hadi kizazi.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza