Kabla Ya Kuomba: Maombi Ni Zaidi Ya Mbwembwe
Ufahamu sahihi juu ya moyo wa Mungu Baba yetu unaomba.
Ni rahisi sana kuona mtu ameokoka leo halafu wakati huo huo anaambiwa aanze kuomba, utafikiri wokovu unakuja na “syllabus” ya maombi ndani ya moyo wa mtu. Watu wengi sana wanaomba lakini si wote wanapata matokeo wakiomba na hawajui kwa nini hawapati matokeo. Pamoja na kwamba watu wengi pia wamefundishwa mbinu za kuomba lakini siyo wote wanaojua mtazamo wa Mungu juu ya maombi. Hii imesababisha watu kuanza kujilaumu kwamba labda hawakuomba vizuri, labda maombi hayakutosha au hata staili yake ya maombi ndiyo isiyo na matunda. Ni mara chache kusikia watu wakizungumzia maombi kwa upande wa Mungu yaani kufahamu moyo wake.
Lengo la kitabu hiki ni kukusaidia kufahamu moyo wa Mungu juu ya maombi yetu na jinsi anavyoyajibu.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza