Kabla Ya Kuingia Kwenye Mahusiano
Kabla ya Kuingia kwenye mahusiano kuna mambo ambayo unapaswa kwanza kuyajua ili usianzishe mahusiano ambayo baadae utakuja kujilaumu ni kwanini ulipuuzia kuyajua mambo ya msingi kabla ya kuingia kwenye mahusiano...
Kabla ya kupika chakula huwa unaandaa vitu vinavyohusika ili uweze kuandaa na kupika chakula kizuri na kitamu kama jinsi ulivyokusudia. Chakula kizuri na kitamu ni matokeo kama jinsi ilivyo chakula kibaya kisicho na ladha pia.
Ndivyo jinsi ilivyo hata furaha katika mahusiano
yako kabla ya ndoa hutegemea zaidi namna ambavyo utakavyoanza na kuendelea kufanya ukiwa kwenye mahusiano hayo na mpenzi wako.
Vijana na watu wengine ambao wana shauku ya kuingia na kuwa kwenye mahusiano huwa
wanataka tu kuingia kwenye mahusiano na kuwa na ndoa pasipo kujua au kujikumbusha kuwa
mahusiano na ndoa nzuri daima hujengwa na watu wanaohusiana vizuri kwa mujibu wa msingi
ambao wameanza kuutengeneza tangia awali.
Kama jinsi ilivyo kwenye kuandaa chakula pasipo kuwa na vitu sahihi na kufuata utaratibu wa kupika basi utajikuta unapika kitu cha ajabu ambacho hautatamani hata kurudia kukila tena.
Mfano unataka kupika dagaa lost ukaanza kuweka maji kwenye sufuria, kisha zikafatia nyanya, kitunguu, chumvi, na mafuta kwa juu. Ni wazi hapa hautapata pishi ulilokusudia kulipata
kwasababu umekosea formula ya kupika dagaa lost.
Ndivyo jinsi ilivyo hata katika mahusiano unapokosa kujua uanze namna gani ili uweze kufanya
maamuzi sahihi kwa kuwa na mahusiano mazuri na unayoyahitaji, basi itakuwia vigumu sana
kuwa na mahusiano yenye furaha na amani ikiwa mwanzo ulianza pasipo kuzingatia vitu fulani
ambavyo nitaenda kuvizungumzia zaidi ndani ya hiki kitabu.
Viungo ambavyo vinafanya pishi liwe tamu ndio sawa na vitu ambavyo nitavielezea
vinavyofanya mahusiano yawe yenye furaha na amani endapo tu utasoma kitabu hiki na
kuzingatia wakati unapotaka kuanzisha mahusiano na mtu yeyote kwaajili ya kuoana, na kujenga familia ambayo kila mmoja anahitaji kuwa nayo.
Endelea kusoma zaidi…
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza