Kabla Pendo Halijanoga
Kabla Pendo Halijanoga
Hivyo, kabla pendo halijanoga na penzi halijakuchanganya basi jitahidi uwe na akili kichwani. Na mambo haya tutakayoenda kujifunza pamoja ni maombi yangu kwako. Ninatamani yakupe kuona kuna umuhimu wa akili yako kufanya kazi katika pendo na hata pale ambapo mmeamua kuingiza na penzi, basi bado akili yako iwe inafanya kazi. Na uwe tayari kuyaishi matokeo ya kila utakachoamua badala ya kutoka kwenye mahusiano na kumlaumu kila mtu. Ukiwa na maarifa sahihi nikujulishe tu mahusiano yatakuwa baraka sana kwako na hata ikifikia hatua wote mmeona mwaweza kuingia kwenye ndoa basi mtafurahi.Hata katika hamsini zenu maana kuna msingi mmeujenga haujaamuliwa na hisia tu ila akili zenu zilifanya kazi.