JINSI YA KUMALIZA UMASIKINI WA KIFAMILIA
Namna ambavyo unaweza kujenga utajiri katika familia yako mapema, na namna ambavyo unahitajika kufikiri ili kufikia hili
Ulishawahi kuwaza ya kuwa leo hii unaweza kununua kiwanja ambacho kinaweza kukugharimu takribani milioni 1 ila miaka 20 baadae hiki kiwanja kinaweza kumfanya mwanao kuishi kama milionea?
Au chukulia leo hii umesoma vitabu 20 na umekusanya ujuzi wa kutosha ambao unakufanya upate matokeo ambayo unayo leo hii, unafahamu ya kuwa unaweza kuuhamisha huu ujuzi na maarifa kwa kizazi kijacho au kwa wanao na wao pia wakapokea matokeo ambayo ni sawa na wewe ili kwa muda mfupi?
Hii inaitwa falsafa ya kusimama juu ya bega la kizazi kilichotangulia, haijalishi umezaliwa katika mazingira ya namna gani unaweza kumaliza kabisa umasikini katika familia yako kwa kiwango cha kuwa kama wewe uliitwa masikini basi kizazi chako au watu wanaokuzunguza unaweza kuwabadilishia jina kirahisi mno
Na hii haitakugharimu chochote bali ni kubadili tu mfumo wako wa fikra na kutumia fursa zilizo mbele yako kama nilivyoeleza katika kitabu hiki JINSI YA KUMALIZA UMASIKINI WA KIFAMILIA
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza