Jinsi Ya Kujenga Ubobevu Wa Kitaaluma
Maalum kwa wanafunzi kwenye ngazi ya vyuo wenye nia ya kunufaika na taaluma zao.
Watu wengi wamekua wakihimiza sana kuhusiana na suala la elimu. Mfumo wa elimu hasa kwa nchi za Afrika unachukua muda mrefu sana wa wanafunzi takribani katika ya miaka 15 -20. Vijana wengi wanatumia muda kuwa shuleni. Changamoto kubwa inajitokeza pindi wanapohitimu masomo yao na kupata fani au taaluma, wanakosa sifa ya KUAJIRIKA. Wengi wao huishia kukata tamaa na hata kujikuta wanafanya vitu ambavyo hawakusomea.
Ukiangalia walio wengi kwenye sekta ya ajira hawafanyii kazi kile walichosomea katika ngazi ya fani, bali kile kilichojitokeza mbele yao.
Kitabu hiki ni mahsusi kwa wanataaluma wote kujenga misingi ya kuwasaidia namna ya kuwa wabobevu katika kile wanachojifunza ili waweze kukifanyia kazi pindi watakapohitimu.
Kitabu hiki ni mwafaka kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali, waalimu, watunga sera na wazazi.
Unaweza kabisa kujenga ubobevu wa kitaaluma kwa kujifunza na kufanyia kazi mikakati iliyoanishwa katika kitabu hiki.
Kitabu hiki kimeandikwa na Adv.Isaack Zake na Daniel Zake