Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako
Nikiwa Mkubwa Nataka Kuwa Nani?
Kumbuka kipindi cha maisha yako, ulipokuwa mtoto, kati ya miaka mitano mpaka 10, hicho ni kipindi ambacho kila mtu alikuwa anakuuliza swali hili; ukiwa mkubwa unataka kuwa nani? Uzuri wa kipindi hicho ni kwamba, ulikuwa mwaminifu, ulikuwa unaeleza kile kilicho ndani yako na hukuwa na shaka yoyote. Ulipoulizwa ukiwa mkubwa unataka kuwa nani, huenda ulijibu bila wasiwasi, nataka mwalimu/msanii/fundi/daktari/polisi/rubani na mengine. kuwa Ulijibu bila ya wasiwasi na bila ya hatia kwa sababu ulijua unavutiwa na nini na uliona wengine waliofika huko na hukuwahi kufikiria kwamba unaweza usiwe kama wao. Uzuri mwingine wa kipindi hicho cha miaka 5 mpaka 10 ni kwamba hata wale waliokuuliza walikubaliana na majibu yako, hawakukukatisha tamaa, hawakukuambia huwezi, walikubaliana na wewe, walifurahi kuwa una ndoto kubwa na waliamini nguvu iliyo ndani yako. Tatizo lilikuja pale ulipoendelea kukua, huku ukiwa kwenye mfumo wa elimu. Ulipoanza kushindanishwa na watoto wengine kupitia mitihani ya darasani, matokeo yako yalianza kutumika kupima ndoto zako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza