Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Jilipe Mwenyewe Kwanza - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali
Best Seller

JILIPE MWENYEWE KWANZA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh. 7,000 Tsh.
Discount Code : B56497o
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
May 29, 2024
Product Views:
1,700
In category:
Sample

DIBAJI JILIPE MWENYEWE KWANZArnMtu yeyote mzima, ambaye amefanya kazi yoyote ya kuingiza kipato, ukijumlisha fedha zote ambazo amewahi kupokea ni nyingi sana kuliko alizonazo. Yaani hata mtu ambaye yupo kwenye madeni makubwa, bado ukijumlisha fedha ambazo amewahi kulipwa ni nyingi.rnSwali kubwa sana la kujiuliza ni nini kinapelekea watu ambao wanaingiza kipato kujikuta wamebaki hawana kitu kabisa? Mwandishi Grant Cardone amewahi kusema alipokuwa na miaka 25 alikuwa na fedha kidogo kuliko alivyokuwa na miaka 11. Akimaanisha akiwa na miaka 25 alikuwa na madeni mengi kuliko alivyokuwa na miaka 11.rnUkweli ni kwamba, licha ya watu kuingiza kipato, bado wamekuwa wanabaki hawana kitu kwa sababu ya kushindwa kujilipa wao wenyewe. Wanakuwa tayari kuwalipa watu wengine wote, lakini wanajisahau wao wenyewe. Mwishowe wanakuwa kama madalali wa fedha zao, wanazipokea na kuzipeleka kwa wengine.rnJambo la kufurahisha ni watu huwa hawakosi sababu kwenye jambo lolote wanalofanya au kushindwa kufanya. Ukimuuliza mtu yeyote anayeingiza kipato kwa nini anatumia chote mpaka kinaisha, anakujibu kipato chake hakitoshelezi. Hivyo akishatumia, habakiwi na chochote cha kujilipa yeye mwenyewe. rnKwa haraka unaweza kukubaliana na sababu hiyo, lakini ni mpaka pale utakaporudi kwenye uhalisia na kugundua kwamba, fedha haijawahi kukosa matumizi. Fedha ikiwepo, matumizi yatapatikana tu. rnKitabu hiki cha JILIPE MWENYEWE KWANZA ni mwongozo sahihi wa kifedha kwa mtu yeyote anayetaka kujijengea uhuru wa kifedha na utajiri kwa kuanzia pale alipo sasa. Kama jina linavyojieleza, zoezi la kujilipa mwenyewe linapaswa kuwa la KWANZA. Yaani unapopokea kipato chako, kabla hujafanya matumizi yoyote, unaanza kwa kutenga pembeni fungu la kujilipa, halafu kinachobaki ndiyo unatumia.

Ni kwa kutumia kanuni hiyo ya KUJILIPA MWENYEWErnKWANZA ndiyo unaweza kujilipa hata kama kipato chako ni kidogo kiasi gani.rnUnapoweka vipaumbele sahihi kwenye matumizi ya fedha zako, kwa kuanza narnkujilipa, unaweza kutumia kipato kidogo ulichonacho kujenga utajiri mkubwa.

Neno utajiri limewatesa sana watu wengi. Waturnwamehangaika na mambo mengi sana kupata utajiri. Wapo walioiba na kudhulumurnwengine, na utajiri walioupata haukudumu. Wapo waliocheza bahati nasibu narnkamari na wengi walikosa, huku wachache waliopata nao wakishindwa kudumu narnutajiri. Na wapo waliotumia njia za kishirikina na bado wasipate utajirirnunaodumu.

Mambo mengi kwenye maisha huwa ni rahisi,rnlakini watu huwa wanahangaika kuyafanya kuwa magumu. Ikiwepo swala la utajiri,rnmahangaiko yote ambayo watu wanayo juu ya utajiri, ni kujitesa tu. Kanuni yarnkujenga utajiri ni rahisi na inayoeleweka na kila mtu. Na inasema hivi; MARArnZOTE MATUMIZI YAWE MADOGO KULIKO KIPATO CHAKO.

Kama utaamua kuachana na mambo mengine yote narnukaamua kukomaa na hilo moja tu, kwamba kwenye kila kipato unachoingizarnmatumizi yawe madogo kuliko kipato hicho na ukaenda hivyo kwa maisha yako yote,rnlazima utajenga utajiri. Huo ni uhakika, siyo kubahatisha. Utawezajernkuhakikisha mara zote matumizi yanakuwa madogo kuliko kipato? Jibu lipo ndanirnya kitabu hiki, kwa kuhakikisha kwenye kila kipato unachoingiza, unajilipa wewernmwenyewe kwanza kabla hujaanza matumizi. Na kile unachojilipa hukiachirnkiholela, bali unakiweka kwenye gereza ambapo huwezi kukifikia kirahisi. Yoternhayo utajifunza kwa kina kwenye kitabu hiki.

Kwenye kitabu cha MTAALA WA UTAJIRIrnnilichoandika, nimeeleza kwa kina kwa nini utajiri au umasikini hauanzii kwenyernkipato, bali kwenye fikra. Na ushahidi wa hili ni watu wawili wanaoweza kuwarnwanafanya kazi au biashara ya aina moja, wanalingana kipato, lakini mmojarnakajenga utajiri huku mwingine akibaki kwenye umasikini. Unaona na kufikiriarnnini ndiyo mahali utajiri au umasikini unapotengenezwa kwenye fikra zako.rnKinachoonekana nje ni matokeo tu.

Kudhihirisha hilo, angalia jinsi ambavyo waturnwengi wanaopata fedha nyingi kwa mkupuo, labda wamepata mirathi, wamelipwarnmafao au kushinda bahati nasibu, huwa wanaishia kuzipoteza haraka pia.

Eng. Tindwa Martin amefanya kazi kubwa yarnkukujengea mtazamo sahihi wa kifedha kwenye kitabu hiki cha JILIPE  MWENYEWE KWANZA. Ni bahati ya kipekee kwakornkupata kitabu hiki, hivyo kisome kwa kina, kielewe na kiweke kwenye matendo.

Matumaini yangu ni baada ya kusoma kitabu hiki,rnhutaichukulia tena fedha kwa namna ulivyokuwa unaichukulia awali. Kwa kilarnfedha inayopita kwenye mikono yako, iwe umelipwa kwa kazi, umepewa zawadi aurnhata umeokota, utaitendea kulingana na mafunzo unayoyapata hapa.

Nikutakie kila la kheri kwenye safari yako yarnkujenga utajiri na uhuru wa kifedha ambayo unaianza kwa uhakika kwa mwongozo warnkitabu hiki. Familia yako, taifa lako na dunia kwa ujumla inahitaji matajirirnwengi. Wewe unapaswa kuwa mmoja wa hao ili uweze kuwa na mchango mzuri kwarnwengine.

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio,rnMwandishi na Mjasiriamali.

rnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrn

www.amkamtanzania.com

ILI UCHUKUE HATUA LAZIMA UWE NA SABABU

Kwenye kitabu hiki ndio maana tumekupa sababu Hamsini ambazo zitakusaidia kuweza kuchukua kwani hata kama umeenda stendi hauwezi kumwambia Konda unaenda kokote ambapo gari inakwenda hivyo ukiwa na sababu itakusaidia kupata majibu ya hatua za kuchukua ili kuweza kujilipa mwenyewe kwenye kila kipato kinachopita kwako iwe Mshahara, zawadi au kipato chochote ambacho umekipata. Kwenye sababu hizi utapata sababu ya kuweza kuchukua. Nakutakia usomaji Mwema na kuchukua hatua kwenye yale uliyojifunza.

Eng. Tindwa Martin

www.jilipemwenyewe.co.tz

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

GetValue Recommendations
Old is Gold