JIKOMBOE NA MADENI
Mbinu na mwongozo wa kukusaidia kutoka kwenye madeni
Kuwa na madeni sio uharifu , hiki ni kitu ambacho wakati mwingine kinaweza kupata hata pasipo wewe kutarajia.
Umeingia kwenye madeni na huwenda ni kwasababu Kuna vitu havikwenda sawa tu kwenye mambo yako yaliyokuwa yanahitaji fedha.
Mimi naamini hapo ulipo Huna haja ya kujilaumu na kujutia sana, Kwa sababu huwezi kubadili jana ila Kule unakoelekea ndiko unakoweza kukubadili.
Sasa unaweza kuamua kuibadili leo Ili uiingie kesho isiyo na madeni, inawezekana kabisa.
Unajua kutoka kwenye madeni uliyonayo ni mchakato unaohisisha matumizi ya mbinu na kanuni mbalimbali zenye nguvu ya kukuletea matokeo chanya kwenye hali Yako ya uchumi.
Kwenye kitabu hiki nimekuandalia Kwa mtililiko na mpangilio mzuri kila kitu unachopaswa kukifahamu na kukufanyia kazi Ili kutoka kwenye hali hiyo ya madeni,
Nimeelezea juu ya mtu unayepaswa kuwa Ili uyaondoe madeni na maarifa unayopaswa uyatumie kwenye maisha Yako Ili usije ukawa mtu wa madeni tena.
Mbinu hizi nimezifundisha Kwa watu kadhaa na zimewaletea matokeo , na wewe unaweza kuwa mmoja wao leo Kwa kununua kitabu hiki. Kwenye kitabu Cha JIKOMBOE NA MADENI, Kuna madini mengi ya kukusaidia ikiwemo,
Kitakusaidia kujua.....
*1::Sababu zinazowafanya watu wengi waingie kwenye madeni mara kwa mara*
*2::Athari za madeni*
*3::Kwanini fedha zako hazitoshi mahitaji Yako*
*4::Dalili hatarishi za kuziangalia kabla hujaingia kwenye madeni*
*5::Maswali ya kujiuliza kabla hujaenda kukopa*
*6::Msaada wa bajeti kwenye kukusaidia kutoingia na kutoka kwenye madeni*
*7::Njia za kukwepa madeni*
*8::Hatua wezeshi za kukusaidia kutoka kwenye madeni*
*9::Kanuni muhimu za kukusaidia kutoingia au kutoka kwenye madeni.*
Na vingine vingi utajifunza kwenye kitabu hiki ambavyo vitakusaidia kupiga hatua kwenye uchumi wako na kukukomboa na madeni.