JIFUNZE LUGHA YA KISWAHILI
JIFUNZE LUGHA YA KISWAHILI ni kitabu kinacho muelekeza mtumiaji wa lugha ya kiswahili kujifunza kusoma na kuandika maneno ya lugha ya kiswahili. Mwanafunzi atajifunza silabi mbalimbali za kiswahili kama vile silabi sahili au huru pamoja na zile silabi changamano. Hali kadhalika kuunganisha silabi moja na nyingine kwa lengo la kupata maneno, umoja na uwingi katika lugha ya kiswahili, kuhesabu namba kwa lugha ya kiswahili na mwisho kusoma habari mbalimbali kwa lugha ya kiswahili Ili kukuza uwezo wa mwanafunzi katika kusoma maandiko mbalimbali ya lugha ya kiswahili.
Pia ni kitabu kinacho lenga kutoa muongozo kwa wanafunzi wazawa wa lugha ya kiswahili na wageni wanaojifunza lugha ya kiswahili kwa mara ya kwanza katika hatua za awali. Kitabu hiki ni msaada mkubwa kwa wanagenzi wa lugha ya kiswahili kwani kimetumia mbinu rahisi ambazo zitamsaidia mwanafunzi kujifunza hata akiwa mwenyewe.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza