Jifunze Kusaidia Wajane Na Yatima
Price:
5,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
May 28, 2021
Product Views:
4,164
Sample
Kitabu hiki ni muongozo wa kupata baraka kupitia kuwasaidia Wajane na Yatima kwa maelekezo ya Biblia. Kitakufaa sana wewe unahitaji kupata baraka za Mungu kwa kuwasidia wengine.
Yapo mambo mengi sana ambayo ni muhimu katika maisha yetu, ambayo tunatakiwa
kuyatekeleza kabla ya muda wetu wa kukaa hapa duniani haujaisha. Na ikiwa mambo hayo ya msingi hatutayatekeleza maisha yetu yote hapa duniani hayatakuwa na maana kabisa.
Pamoja na majukumu mengi uliyo nayo katika dunia hii,hili jukumu usilisahau kabisa. Jukumu lenyewe ni kuwasaidia wajane, yatima na wasiojiweza. Biblia haimuungi mkono mtu yoyote duniani ambaye atatoa udhuru wa kutekeleza jukumu hili. Jambo hili si kwa mkristo tu bali ni kwa kila mwanadamu aliyejaliwa kuishi. Jambo hili limeonekana kama utumishi mdogo sana duniani lakini ni utumishi mkubwa sana mbele za Mungu. Mungu amenipa ujumbe huu nikufikishie sio kwa bahati mbaya hapana ni kwa makusudi kabisa. Unaweza kudhani ni bahati mbaya tu kitabu hiki kukufikia mkononi mwako la hasha ni makusudi kabisa ya Mungu ukipate ili ukisome na upate ujumbe huu. Usichoke rafiki jitahidi usome hakika utaelewa vizuri.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza