JIFUNZE BIBLIA Toleo La 1
JIFUNZE BIBLIA Toleo la 1
UTANGULIZI.\\r\\n
Waandishi mbalimbali wa Biblia, Mungu aliwatumia kusisitiza nguvu juu ya nguvu iliyomo katika \\r\\nNeno la Mungu au Biblia. Neno la Mungu li hai, linadumu milele, ni uzima, linaponya, linaokoa; \\r\\npia kwa Neno vitu vyote vya dunia viliumbwa, na imani yetu tunajenga juu ya Neno la Mungu. \\r\\nKwa sababu hiyo, manabii wanasisitiza nguvu ya Neno la Mungu (Yer. 23:28,29); wafalme nao \\r\\n(Mith. 30:5,6); Mitume nao (Kol. 3:16; 2Tim. 3:16; Waeb. 4:12,13); na Yesu mwenyewe (Math. \\r\\n5:18; Yoh. 6:63; 12:48).
Yesu katika kuliacha Kanisa duniani, alitoa wengine wawe Mitume, wengine wawe manabii, \\r\\nwengine wawe wainjilisti, wengine wawe wachungaji, na walimu kwa kusudi la kuwakamilisha \\r\\nwatakatifu (Waefeso 4:11,12); maana yake ni kwamba huduma ya utume, huduma ya unabii, \\r\\nhuduma ya uinjilisti, huduma ya uchungaji na huduma ya ualimu, zote zinajengwa katika Neno \\r\\nla Mungu. Ingawa mwalimu anaonekana ni wa mwisho katika orodha ya mtume Paulo, lakini \\r\\nijulikane kwamba, pamoja na kwamba huduma zote zina muhimu ulio sawa kwa Kanisa, lakini \\r\\nhuduma zote zinalala juu ya mwalimu. Huduma zote zinajengwa katika msingi wa mafundisho. \\r\\nIli wakristo wawe imara wanahitaji kupokea mafundisho ya kutosha na yaliyo sahihi. Kazi hii \\r\\nhawezi kuifanya mchungaji peke yake, bali anahitaji kuwainua watu waaminifu Kanisani, na \\r\\nkuwekeza kwao Neno la Mungu ili waweze kusaidia kufundisha wengine (2Tim. 2:2).
Kulingana na Neno la Mungu, mtume katika huduma yake anahitaji kufundisha, mwinjilisti \\r\\nkatika huduma yake anahitaji kufundisha, nabii na mchungaji kadhalika. Mwalimu ana jukumu \\r\\nkubwa kutoa mafunzo hata kwa huduma nyingine. Mtume asipofundishwa kazi yake, au nabii, \\r\\nau mwinjilisti, hawezi kuwasaidia watu. Mhubiri anayehubiri kwa kufundisha ana mafanikio \\r\\nzaidi katika huduma yake. “Na ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida na maji ya msiba, \\r\\nlakini waalimu wako hawatafichwa tena, ila macho yatawaona waalimu wako; na masikio \\r\\nyako yatasikia neno nyuma yako, ikisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa \\r\\nkulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto” (Isa 30:20,21).
Nabii Hosea alisema, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” (Hos. 4:6). Wakristo \\r\\nwengi wamejaa ujinga wa kiroho kwa sababu ya kukosa mafundisho, na si mafundisho tu, bali \\r\\nmafundisho yaliyo sahihi (2Kor. 2:17; 4:2; 1Pet.2:2). Kuna mafundisho mengi yanayofundishwa \\r\\nmakanisani yameghoshiwa, na hivyo hayawezi kumtia mtu afya ya kiroho. Kughoshi maana yake \\r\\nni ‘kuchanganya’ na kitu kingine. Mafundisho mengi yamechanganywa na mila na desturi, \\r\\nmawazo na matakwa ya watu, hisia na ujanja wa watu. Mtoto anayekunywa maziwa ambayo \\r\\nyamechanganywa na maji hudhoofika afya yake; kadhalika anayepokea mafundisho ambayo \\r\\nyamechanganywa na mapenzi ya wanadamu huwadhoofisha watu kiroho. Neno la Mungu \\r\\nlinaitwa kweli, upanga wa Roho, moto, nyundo, maji safi, maziwa yasiyoghoshiwa n.k. \\r\\n