ITAFUTE ANWANI YAKO
Katika dunia iliyojawa watu wa kila aina wenye vipawa, uwezo na ujuzi mbalimbali wewe bado niwa toafuti, umetengenezwa na kuumbwa ili kuwa jibu la tatizo ambalo flani katika kizazi chako. Liko eneo maalumu ambalo umeandaliwa ili utawale na kumiliki ili kutimiza shauku na ndoto kubwa aliyokuwa nayo Muumbaji wako. Umepewa vipawa na uwezo mbalimbali ili kukuwezesha kujua ni wapi unapamudu sawasawa, na hiyo ndio Anwani yako ya maisha. Ni Wakati wa kuitafuta.
Je! Akili yako imekuwa ikifikiria mambo mengi yasiyogusa maisha ya wengine na kuyaweka maisha yako katika nafasi unayoitamani kwa muda mrefu? Iweke akili yako katika njia inayoelekea ushindi. Unaweza kumiliki vyote unavyoviwaza na kukuwezesha kuitambua anwani yako.
Kuitambua anwani yako ya maisha ni kulitambua eneo la milki yako. Huwezi kufaa na kuwa bora katika kila eneo, isipokuwa eneo lile tu unaloendana nalo. Ni jukumu lako kuitafuta na kuitambua anwani yako ili kujiweka sawa na kusudi lako. Kuishi nje ya anwani yako ya maisha kutakufanya upishane na kusudi la aliyekuumba na kukuleta duniani.
Kitabu hiki kitakuwezesha kujua wapi pa kuanzia na nini cha kufanya ili kuitafuta na kuitambua anwani yako ya maisha.
• Umepangiwa jambo gani?
• Nguvu ya kutokata tamaa
• Namna ya kuiendea baadaye yako
• Maajabu/nguvu ya maneno yako
• Jinsi ya kutoka nje ya eneo lako la kujiamini
Matamanio makubwa ya binadamu yeyote ni nguvu ya kufikia malengo yake na kuleta tija katika maisha yake. Kuifikia nguvu hii ni lazima kuwa katika nafasi ya sahihi.
Methali 24: 33 - 34 “Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!. Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza