ISHARA 12 ZA KUWATAMBUA MANABII NA WAALIMU WA UONGO
Suala linalohusu kuwatambua manabii na waalimu wa uongo, limekuwa linaleta shida sana kwa watu wengi, kwa sababu manabii na waalimu hao wa uongo wanapokuja kwa watu kuleta ujumbe wao hudai “tumetumwa na Mwenyezi Mungu kuleta ujumbe wake na hivyo kuwataka wanadamu kuupokea, kuuamini na kuufuata”. Inapotokea nabii au mwalimu amekuja kwa mtindo huo na akakutana na watu wasiojua kuwapambanua manabii na waalimu kwa misingi ya Neno la Mungu, ndipo ukengeufu hutokea, na makundi ya aina mbalimbali ya imani za uongo hujitokeza. Hivyo lengo la kitabu hiki ni kukupa maarifa katika msingi wa Neno la Mungu, kuweza kuwatambua manabii na waalimu wa uongo.
Rafiki yangu mpendwa,
Nakushauri na kukusihi usome kitabu cha ISHARA 12 ZA KUWATAMBUA MANABII NA WAALIMU WA UONGO, kwani ni kitabu kilichosheheni maarifa mtambuka kwa nyakati tulizo nazo kuhusu Manabii na Waalimu wa uongo.
Kitabu hiki ni cha Kiroho na kimeandikwa katika misingi ya Biblia Takatifu. Kitabu hiki kimeandikwa kwa kurejerea vifungu mbalimbali kutoka katika Biblia ambavyo vitakupa tafakari ya kina inayoakisi hali halisi ya maisha ya sasa hususani juu ya utambuzi wa manabii na waalimu wa uongo.
Rafiki, Natamani sana usome kitabu hiki kutokana na ujuzi, utambuzi na ufahamu utakao upata mara baada ya kusoma kitabu hiki. Miongoni mwa mambo utakayojifunza katika kitabu hiki ni kama ifuatavyo;
Maana ya unabii na ualimu
Sifa za Mwalimu wa Neno la Mungu
Unabii wa uongo Unaletwa na nani?
Ni kweli wapo manabii na waalimu wa uongo?
Utawatambuaje manabii na waalimu wa uongo?
Njia za kupona dhidi ya manabii na waalimu wa uongo
Pia maarifa utakayoyapata katika kitabu hiki yatakusaidia kuepukana (kuwasaidia wengine kuepukana) na wimbi la sasa la watu kutangatanga katika imani na madhehebu tofautitofauti kwa lengo la kutafuta miujiza na mafanikio. Kwa kusoma kitabu hiki utakuwa na msimamo thabiti katika imani.
Karibu sana rafiki yangu mpendwa, pata nakala yako uondokane na uangamivu kwa kukosa maarifa juu ya Manabii na Waalimu wa uongo.