INAWEZEKANA2
ISHI ZAIDI YA ULIVYOISHI WAKATI ULIOPITA
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa makala arobaini na mbili zenye dhamira ya dhati ya kufundisha, kuonya, kukumbusha, kuhamasisha, kutia moyo, kushauri na kuburudisha. Lengo kuu la makala hizi ni kuambukiza mtazamo chanya kwa jamii (wasomaji) utakaopelekea hatua mbele zaidi katika mafanikio ya kimaisha katika maeneo mbalimbali ambayo wamejikita.
Makala hizi zimeandikwa kama matokeo ya mafunzo mbalimbali ambayo mwandishi amekuwa akiyapata kutoka kwenye mazingira halisi kwa kuona, kuhisi na mengine kama sehemu ya ushuhuda wa yale ambayo yametokea katika maisha yake akiwa katika harakati za kupambana kutafuta uhalisia wa ndoto zake. Lengo kuu la kuzingatia mazingira halisi sanasana yale ya kitanzania ni kuwawezesha wasomaji (jamii) wa namna mbalimbali kuelewa kwa urahisi zaidi mambo ambayo kama watachukua hatua kuyafanyia kazi yanaweza kuwapa hatua zaidi katika mapambano ya kufikia ndoto zao au kutimiza mipango yao maishani.