IJUE NA UISHINDE HOFU INAPOKUWA KIKWAZO CHA MAFANIKIO YAKO
“Malengo yanaweza kuwa ngazi kwenye mafanikio yako, lakini hofu inaweza kukuzuia.”
Hofu katika maisha yetu ni moja ya vikwazo vikubwa katika kuyafikia mafanikio ya kweli. Vyanzo vya hofu ni vingi ila msingi wake ni hisia hasi ambazo mtu ameshindwa kuzidhibiti kwa wakati. Kuijua na kukabiliana na hofu ni jambo zuri katika maisha. Hofu mbaya si tu ni kikwazo, bali pia hukwamisha mpango wa Mungu katika maisha yetu. Jinsi gani tunaweza kukabiliana na hisia mbaya za hofu kwa ufanisi na kuweza kufanya maamuzi mazuri na yenye uhalisia? Hatua zipi tunaweza kuzichukua ili kukabiliana na hofu? Maswali haya na mengine mengi yameweza kupewa majibu kupitia maudhui ya kitabu hiki ambayo yameandaliwa kwa mtiririko mzuri. Mungu aendelee kukubariki na kukuwezesha ujifunze, kupata na kuyatumia maarifa katika kutekeleza malengo na hatimaye kulifikia kusudi.