Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ifanye Pesa Yako Kuwa Ng%E2%80%99ombe Wa Maziwa - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

Ifanye Pesa Yako Kuwa Ng’ombe Wa Maziwa

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
8,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Oct 02, 2024
Product Views:
177
In category:
Sample

Ifanye Pesa Yako Kuwa Ng'ombe Wa Maziwa ni kitabu ambacho kinakupatia maarifa na mbinu ambazo unaweza ukazitumia kutengeneza kipato chako ili kuanza kuishi maisha huru kifedha...

Ifanye Pesa Yako Kuwa Ng'ombe Wa Maziwa ni kitabu ambacho kinakujengea ujasiri wa kifedha na kukupa mbinu mbali mbali ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupata pesa na kuitumia pesa yako ili kuishi maisha huru.

Kila mtu yupo bize kutafuta maisha kwa matarajio ya kuwa ipo siku atapumzika na kufurahia kazi ya mikono yake kama vile Mwenyezi Mungu alivyofurahia kazi ya uumbaji wake ndani ya siku sita [Mwanzo 1: 31] na kisha akapumzika siku ya saba [Mwanzo 2:2].

Kwa maana hiyo hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho hata katika utafutaji; yatupasa tuone kabisa ya kuwa tunapaswa kufanya kazi ndani ya muda fulani kisha tufurahie kazi ya mikono yetu.

Uhuru wa kifedha ni matokeo ya kufanya kile ambacho umekuwa ukikifanya kwa kuweka malengo kuwa baada ya muda fulani utastaafu kufanya jambo fulani ukiwa na uhakika wa kuishi maisha yako pasipo na kuwa na mashaka juu ya masuala ya kifedha.

Ikiwa Mwenyezi Mungu alijiwekea muda wa kufanya kazi zake kisha akapumzika ili afurahie kazi ya mikono yake, vipi kuhusu wewe ni malengo gani umejiwekea ili ustaafu kufanya unachokifanya ukiwa na uhuru wa kufanya jambo lolote ulipendalo wakati wowote?

Kama tujuavyo kuwa hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho, hivyo kufanya kazi kwa bidii na kujiwekea malengo yako ni jambo zuri sana kwasababu umri wa binadamu umegawanyika sehemu tatu, umri wa kujifunza, umri wa kutafuta, na umri wa kupumzika.

Kitu ambacho binadamu wengi hawajawahi kukiweza ni kipindi cha kutumia pasipo kutafuta, yani wengi wamekuwa wakitafuta na kutafuta mpaka siku wanarudi mavumbini wakiwa hawajapumzika katika utafutaji wa pesa.

Kupitia kitabu hiki utapata kujifunza nini maana ya kutafuta pesa ili ufikie uhuru wa kifedha na sio kutafuta pesa mpaka umri wa kupumzika. Kimeelezea zaidi namna ya kuweka malengo ya kifedha ili kufikia uhuru wa kifedha kwasababu pasipo uhuru wa kifedha hakuna uhuru wa maisha.

Ni kitu ambacho kipo wazi kuwa tupo hapa duniani tukiwa na miili hii ambayo inahitaji kutunzwa na kitu pekee cha kuiwezesha ni pamoja na kuwa na pesa, sio pesa tu, bali pesa nyingi ambayo itakufanya uishi maisha bila wasiwasi wa aina yoyote.

Kitabu hiki ni jibu la kwanini watu wengi wanatafuta pesa lakini hawafikii uhuru wa maisha. Yaani wamekuwa wakitafuta pesa miaka nenda rudi pasipo kufikia hatua ambayo itawafanya wakae na kufurahia kazi ya mikono yao baada ya kuvuja jasho ndani ya kipindi fulani.

Ikiwa lengo la utafutaji ni kupata, lakini cha ajabu wengi wamekuwa wakitafuta na kupoteza pasipo na kujua kuna baadhi ya tabia ambazo wapo nazo na hawawezi kuziacha sababu hawajui kuwa ndio chanzo cha wao kuendelea kutafuta pesa pasipo kufikia uhuru wa kifedha.

Ili na wewe usiishi hivyo yakupasa ufanye na kuzingatia yafuatayo.

Endelea kusoma zaidi...

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold