Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Huduma Kwa Wateja Customer Care Silaha Yako Unapoyaendea Mafanikio - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

HUDUMA KWA WATEJA CUSTOMER CARE SILAHA YAKO UNAPOYAENDEA MAFANIKIO

0.2
1
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Feb 26, 2025
Product Views:
195
In category:
Sample

Kitabu hiki ni muhimu sana kwenye taasisi yeyote inayohitaji kukua na kufikia mafanikio, mteje siku zote ni mfalme na kila mteja anahitaji red carpet hata kama anaonekana hana sifa Leo, kesho anaweza kuwa muhimu sana

Wazo la kitabu hiki lilitokana na semina ya huduma kwa wateja ambayo binafsi nilikuwa mshiriki. Hii ilifanyika tarehe 09 na 10/03/2013 hapa VETA Kagera ikiwahusisha wafanyakazi wote wa VETA Kagera na wa Chuo cha ufundi Stadi Ntoma vyote vya mkoani Kagera.

Mwezeshaji Bw. Jerome A. Mwarusha, kipindi hicho akiwa Mkuu wa chuo VETA Kagera, kupitia programu za Connections kutoka Marekani, aliibua tashwishi yangu ya kujifunza zaidi na zaidi katika kutoa huduma bora kila mahali. 

Tangu hapo nimejifunza kwamba huduma bora kwa wengine ni jambo pana na kweli ni la lazima mtu ukalielewa kwa mapana yake ili uweze kusonga mbele hata kuyafikia mafanikio.

Robert Kiyosaki hupenda kusema kwamba watu tukijifunza na kuielewa falsafa ya utoaji tutafanikiwa. 

Anasema kama unataka kila mtu unayekutana naye awe ametabasamu mbele yako, anza wewe kutabasamu, utamwona kila mmoja amekurudishia tabasamu hili hilo. 

Kwenye huduma bora vilevile tutumie falsafa hii hii ya kutoa. Kwamba toa huduma bora kila ulipo  utajikuta unazungukwa na watu wenye ari ya kukuhudumia kwa ubora kabisa. Na hapo utaweza kufanya kila unalolifikiria na ukafanikiwa.

Kumbuka huwezi kufanikiwa bila msaada wa watu, Eric Shigongo ameandika kwenye kitabu chake kinachoitwa Umasikini hadi Mafanikio.

Elimu ni ufunguo wa maisha! Lakini watu wengi tunadhani elimu inayofungua maisha ni ile ya kujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Kwa hakika elimu iliyozungumziwa kuwa inayafungua maisha ni ile inayokuwezesha kufurahia unachokifanya kwa sababu watu wote wanaokuzunguka wanakupa mrejesho chanya. Jambo hili haliwezi kutokea lenyewe bila sababu. Pengine unayo sababu ya kununa, lakini tambua wakati wote ni sababu yako wala haiwahusu wao hata kama unadhani watakuwa wameisababisha.

Elimu ya huduma bora kwa wateja ni mtaji, ndiyo elimu inayokuonesha kuwa unajua namna ya kuishi na watu, na hiyo ndiyo ufunguo wa maisha. 

Itakufungulia pale ambapo mafanikio yako,(kama kupata ajira, nyongeza ya maslahi, kufanikiwa kibiashara, kupanda cheo, kupata msaada wowote n.k), yalikuwa yamefungiwa ukaendelea kubaki ukilalamika kila kukicha.


Hii ndiyo sababu kitabu hiki kinamfaa kila mtu; mwalimu, mwanafunzi, daktari, fundi, mwanamichezo, mjasiriamali, hakimu, dereva, kondakta, mkulima, mtoza ushuru, muuza baa, n.k. ili tu sote tuweze kutoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu. 

Kitabu hiki kinafaa kutumika kama rejea (reference) kwa walimu na wanafunzi katika nyanja za huduma kama usimamizi wa hoteli na uongozaji watalii, taaluma ambazo zina nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira nchini mwetu.

Kitabu hiki kimeandikwa ili kiwemo kwenye kila maktaba ya chuo chochote cha Ufundi stadi nchini ili kuwapa elimu hii wanachuo wetu wazijue mbinu za huduma bora. Hii itawasaidia kufanya vema katika shughuli zao watakazozifanya mara baada ya mafunzo yao.

Vitabu vingine vya Samwel B. Mayala ni

1. Sindano tano za masaa. Kitabu kinachozungumzia kanuni Tano za pesa.

https://www.getvalue.co/prod/sindano_tano_za_masaa_kitabu_kinachozungumzia_kanuni_tano_za_pesa

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold
7,000 Tsh.

Sold by: Sadick Nzania

10,000 Tsh.
(2)

Sold by: MERINA DUGO

10,000 Tsh.

Sold by: Jacob Mushi

300 Tsh.

Sold by: LEMY ZADOCK