HISTORIA YA WAKAGURU
Wajue Wakagulu, mila na desturi zao. Jando na unyago. Welekwa, ikungugo na mlongo na mengine mengi.
Kupata taarifa za wakaguru au wakagulu sasa kumerahisishwa\r\nsana. Kitabu hiki kimesheheni taarifa zote muhimu za wakagulu ambazo zinaweza kuwa msaada sana kwa watu wanaofanya tafiti mbalimbali za makabila. Sasa taarifa hizi zinapatikana kwenye kitabu hiki. Kuna taarifa nyingi za makabila\r\nmbalimbali ya hapa Tanzania na kwingineko duniani kutokana na juhudi\r\nzilizofanywa na watu wa makabila hayo au wengine waliofanya utafiti katika kuziandika.\r\nKwa miaka mingi, hakukuwa na kitabu kilichoandikwa kuhusu Habari za wakaguru katika\r\nmaeneo yote. Baadhi ya watafiti waliandika vipande vipande tu kuhusu wakagulu.\r\nKitabu hiki ni cha kwanza kuwa na taarifa zote muhimu za wakagulu.
Kama zilivyo jamii nyingi za Afrika, wakagulu wana mila na desturi mbalimbali ambazo zimekuwa dira ya Maisha ya kila siku. Kuna mambo\r\nmengi ambayo hivi sasa hayafanyiki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mwandishi wa\r\nkitabu hiki amekusanya taarifa zote hata kama kuna ambazo hazifuatwi katika\r\nmiaka hii. Ni muhimu kuhifadhi kumbukumbu hizi kwa ajili ya kizazi hiki na\r\nvizazi vijavyo. Wako watu wangependa kujua Maisha ya mababu zetu wa zamani walivyokuwa na harakati zao mbalimbali za kutafuta riziki zao.Kama umewahi\r\nkusoma Habari za sultani Mangungo wa usagara, basi utamjua zaidi kwenye kitabu hiki. Wako watawala wengi wa kutoka jamii ya wakagulu ambao wamelezwa kwenye\r\nkitabu hiki lakini huwezi kuwakuta katika maktaba zetu na kwenye vitabu vya historia nya nchi yetu. Kwenye kitabu hiki utawajua na wako wengine wengi tunazidi kuwatafuta na hatimae tutakuwa na orodha ndefu ya watawala wa wakagulu .
Je, unajua kwamba wakagulu hawakuchukuliwa kwenda utumwani na waarabu? Kwenye kitabu hiki utajifunza ni kwa nini wakagulu hawakuwa wahanga wa biashara ya utumwa. Je, jando na unyago katika jamii ya wakagulu vilikuwa vinafanyikaje? Unaamini kwamba kuna watu wanaweza kuzuia na kutengeneza mvua?Yako mambo mengi sana ya kufurahisha na kushangaza katika kitabu hiki.Tumekusanya taarifa za wakaguru tangu karne ya 17 na bado tunaendelea kuzitafuta . Lakini pia katika kitabu hiki kuna taarifa za makabila karibu yote ya Tanzania na baadhi ya nchi zingine za Afrika na kwingineko duniani. Kwa hiyo wakagulu na wasio wakagulu wana mengi ya kujifunza katika kitabu hiki. Karibu sana