HISTORIA HALISI YA MTUME MUHAMMAD SAW
HISTORIA HALISI YA MAISHA YA MTUME MUHAMMAD (SAW) Ni kitabu bora sana kwa Historia za dini kuu mbili, Kikristo na Kiislamu. Katika kitabu hiki utaelewa mengi yanayoshindaniwa na dini hizi Kuu mbili. Aidha kweli nyingi za Kihistoria na vielelezo vyenye kuweka ushahidi bayana kwa yale yote yanayoleta utata. Kitabu kitamsaidia Mkristo na Mwislam. Kitabu kina muhtasati wa Quran nzima nk. Ni moja ya Vitabu pendwa na vinavyotafutwa sana na wasomi wengi.
HISTORIA
HALISI
YA
MAISHA YA MTUME MUHAMMAD (SAW)
KUHUSU KITABU.
Kitabu hiki cha Historia Halisi ya Maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w) ni kitabu muhimu sana kwa kila apendaye kujifunza Historia za dini. Kitabu hiki kimebeba mambo mengi ya Kihistoria kuanzia Adamu, Ibrahimu, Isaka, Ishmael, hadi Israel (Yakobo) na Yesu na Muhammad.
Kitabu hiki ni kitabu cha kipekee katika masuala ya Historia za dini mbili yaani dini ya Kikristo na dini ya Kiislamu. Kitabu hiki kimekusanya mambo mengi zaidi kuliko vitabu vingi uvijuavyo wewe hasa vile vinavyozungumzia Historia za dini hizi mbili. Tunaamini kuwa, kitabu hiki ni moja ya vitabu bora zaidi ambavyo vinavyoshika rikodi ya juu kabisa kwa ubora na umahili wa uandishi wake na uchumbizi wake. Kitabu hiki, kina vielelezo vya kijiografia pamoja na ramani za maeneo yaliyotajwa katika vitabu vya Quran na Biblia.
Kitabu kitamsaidia Mkristo kuijua Historia ya mababa wa imani katika Biblia na kumuongezea uelewa wa kuifahamu Biblia vizuri, pia kitabu kitamsaidia Mwislamu kuifahamu Quran vizuri kuliko pale mwanzo alipokuwa akiisoma, kwani kuna muhtasari wa Quran yote na muhtasari wa baadhi ya Hadithi na malengo yake.
Kitabu kina ushahidi ulio wazi ambao utaondoa utata kuhusu mambo kadha yanayobishaniwa na Wakristo na Waislamu. Kwa mfano, Al Kaaba nani hasa aliyeijenga je ni Ibrahimu? Na je Safaa na Marwa ndipo alipokimbilia Hajiri Mjakazi wa sara? Kitabu kitajibu hoja tata na ngumu ambazo zimewatatiza wengi kuzijibu.
Aidha kitabu kitatoa Historia ya uandishi wa Quran na jinsi ya mchakato wake ulivyokuwa, na kutoa vielelezo kadha kuthibisha kuwa Quran hii ya sasa je ndio ile ya asilia?
Aidha kitabu hiki kimekusudiwa kwa kutumika kwa dini zote na hata wasiokuwa na dini. aidha kitabu hiki kitawafaa zaidi wanafunzi wa vyuo vya Biblia na vyuo vya Kiislamu. Aidha kitabu hiki kitawafaa wasomi na watafiti wa historia.
KUHUSU MWANDISHI.
Mwandishi ni mbobezi wa utafiti wa mambo ya kihistoria, ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika tafiti za masuala ya kidini hasa ya Wakristo na Waislamu. Aidha ameandika zaidi ya vitabu 23 hadi sasa.