HISIA ZA UPWEKE
Watu wote kwa wakati fulani tumewahi kujisikia wapweke. Haiwezekana kumpata mtu ambaye wakati wote amejisikia kueleweka na kutosheka kikamilifu. Upweke ni hisia ya kuachwa pekee yako. Unaweza kuwa kanisani, katika mahusiano ya ndoa, katikati ya kundi la watu na bado ukawa ni mpweke. Upweke linaweza kuwa ni somo lenye kuabisha ambalo hatutaki kulizungumzia au kulikubali. Bado kwa kiasi fulani sote tuna uzoefu nalo, kwa sababu upweke ni matokeo yasiyokwepeka ya anguko la mwanadamu. Upweke hujidhihirisha kama kuugua ndani ya moyo, utupu au kunatamani upendo. Madhara yake ni mambo kama kujihisi kutokuwa na maana na kutokuwa na kusudi lolote maishani. Ishara nyingine mbaya ya upweke ni majonzi na huzuni nzito. Je, Wewe ni mpweke? uko peke yako? Umeachwa?, umetupiliwa mbali ? una huzuni na uzito rohoni kwa kukosa watu wa kukaa nao? Basi mkononi mwako unacho kitabu ambacho kitakusaidia na kukuponya nafsi yako.
YALIYOMO
Ukurasa
• Kutabaruku.....................................
•Shukurani..........................................
•Utangulizi................................ ….…
1.
Hisia
za upweke
2.
Aina
tofauti za upweke
3.
Chanzo
na sababu za upweke
4.
Athari
za upweke
5.
Ufahamu
kuhusu upweke
6.
Kuponywa
na kuwekwa huru dhidi ya upweke
7.
Vitabu
vya rejea
8.
Kuhusu
mwandishi