HISIA ZA WASIWASI
Hisia za wasiwasi ni moja ya hisia mbaya zisizofurahisha zenye nguvu sana zinazo sababisha maumivu ya nafsi na kuwatesa watu wengi. Hisia za wasiwasi au kusumbuka zinaonekana kuwa ni pigo kwa watu wengine leo katika ulimwengu wetu. Ni asili ya binadamu kujali kuhusu hali mbaya katika maisha yetu binafsi, lakini tusipokuwa waangalifu, Shetani atatusababisha kuwa na wasiwasi zaidi ya zile sababu zinazofaa. Wasiwasi ni kitu kinachosababisha ujisikie kufadhaika na kusumbuka hasa katika akili yako. Ni hisia unazozipitia ukiwa unajali sana juu ya jambo fulani ambalo hata bado halijatokea. Katika Mathayo 6: 31- 33 Yesu anatufundisha kwamba hatupaswi kuwa na wasiwasi bali tutafute kwanza ufalme wake na hayo mengine yanayotupa wasiwasi Mungu Atashughulikia. Ikiwa unakabiliana na hali ya wasiwasi, basi tafuta tiba mapema ya chanzo na mzizi wa wasiwasi wako kabla haujakupa pigo baya. Unaweza kuacha kuwa na wasiwasi kwa kufuata tiba iliyopo katika Neno la Mungu. Kitabu hiki kitakusaidia kupata uponyaji wa nafsi dhidi ya hisia za wasiwasi na kuwasaidia wengine ambao wanahitaji uponyaji wa nafsi kwa sababu ya hisia kuonewa na kukandamizwa na hisia za wasiwasi.
YALIYOMO
Ukurasa
Kutabaruku.....................................
Shukurani..........................................
Utangulizi................................
1. HISIA ZA WASIWASI NINI?
2. UFAHAMU KUHUSU WASIWASI
3. MAMBO YANAYO SABABISHA
WASIWASI
4. MADHARA YA WASIWASI
5. UHUSIANO WA WASIWASI NA
MAGONJWA
6. SABABU ZA KUTOKUWA NA
WASIWASI
7. JINSI YA KUKABILIANA NA
KUUSHINDA WASIWASI
8. VITABU VYA REJEA
9. KUHUSU MWANDISHI