HEKIMA YA MUNGU KWA NJIA YA MIFANO
Toleo la pili
Mifano ni nini?
- Mifano ni simulizi fupi za kutunga ambazo hutumika kueleza kweli mbali mbali za kimaisha.
- Mifano ni njia rahisi ya kutumia mazingira yaliyopo kuwawezesha wasomaji ama wasikilizaji kuweza kuelewa kirahisi jambo ambalo lingekuwa gumu kulielewa kwa wepesi.
Kufundisha kwa kutumia mifano, ni mojawapo ya mbinu makini ya kufundishia ambayo humwezesha mwanafunzi kuelewa vyema na kukumbuka kirahisi ukweli uliofunuliwa kupitia kielelezo.
Ufundishaji kupitia mifano ndiyo mbinu kuu aliyokuwa akiitumia Bwana Yesu mara zote kufundishia, hadi ikafikia wakati wanafunzi wake wakahoji inakuwaje anapenda kufundisha kwa mifano (Mathayo 13:13, 34).
Mfalme Sulemani aliyekirimiwa na Mungu Hekima ya hali ya juu mno kiasi kwamba alifanyika kuwa kituo cha utalii, watu kutoka mataifa mengi wakaja kuisikiliza Hekima yake, naye alikuwa akifundisha pia kwa njia ya mifano. Miongoni mwa vitabu vingi alivyoviandika, alitunga pia jumla ya mifano elfu tatu (1Wafalme 4:32).
Karibu ufuatane na Mwalimu Alex E. Bubelwa, mwandishi wa kitabu hiki, si tu kwamba utafurahi na kuburudika, lakini pia utajifunza mengi na ni hakika Mungu atasema na wewe. Kitabu hiki ni nyenzo bora na muhimu sana kwa Walimu wa Neno la Mungu, Wachungaji na kwa mwili wote wa Kristo.
Mungu na akutuanze, nakutakia tafakari njema.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza