HEKIMA YA FEDHA
Hazina ya ufahamu sahihi juu ya fedha
Huwa fedha yangu inakwenda wapi?
Hili ni swali ambalo hata mimi lilinisumbua kwa muda mrefu, nilitumia nguvu sana kuitafuta lakini ilipofika mikononi mwangu, haikulipa ile gharama niliyotumia kuitafuta.
Fedha haikukaa kwenye mikono yangu, fedha haikutosheleza mahitaji yangu ya muhimu, kila nilipoipata na matatizo yaliongezeka pia.
Huwenda na wewe unapitia changamoto kama hii, usijali , hujalogwa wala huna mikosi ya fedha ila kuna kanuni na masharti muhimu ya fedha unapaswa uyafahamu ili uweze kuimiliki fedha yako uipatayo kwa furaha.
Katika kitabu hiki nitakufunulia siri hizo na jinsi ya kuzitumia kudhibiti fedha yako.
Katika kitabu cha HEKIMA YA FEDHA, kuna mambo kadhaa muhimu ya kujifunza.
1:: *Ufunguo wa mafanikio ya fedha*
2::*maongezeko ya fedha ni matokeo ya kufuata kanuni, ijue kanuni ya maongezeko*
3::*Ifahamu HEKIMA YA FEDHA*
4:: *Jifunze funguo nyingi za mafanikio Kwa sababu kila ufunguo una Siri zake*
5::*Kwanini fedha inabadilika thamani*
6::*Namna wazo linavyoweza kukuzalishia fedha*
7::*Zijue sumaku za kuivutia fedha kwako*
8::*Umasikini upo ila sio Kwa ajili yako, namna ya kujitoa na kumilikiwa na Umasikini*
9::*Kanuni za kukufanikisha kwenye fursa za kupata fedha*
10::*Tambua fursa na nyakati*
11:: *Jifunze kanuni ya thamani ikufanikishe umiliki kuiongeza thamani ya fedha yako*
12:: *Zijue sheria za maongezeko ya fedha*
13:: *Kwanini hata wafanyakazi wa benki nao hufa maskini?*
14:: *Siri zilizojificha nyuma ya fedha zinazopotea, haujui fedha zako zinakwenda wapi*
Na vingine vingi utajifunza kwenye kitabu hiki.