Hazina Yako Na Kizazi Chako
Hazina Yako Na Kizazi Chako
Maisha yetu yamefungwa katika nyakati na majira. Hapa ninamaanisha kuna vipindi vya Maisha. Na kwa urahisi ninaweza kusema kuna kipindi kilichopita, kilichopo na kijacho. Kwa kulifahamu hili ni muhimu kutambua kuwa hakuna tunachoweza kubadilisha kwenye yale tuliyokwisha kuyafanya kwenye kipindi kilichopita. Haijalishi hatuyapendi kwa kiwango gani, lakini maadam tumejaliwa kuwa na wakati uliopo, tuna wajibu wa kufikiria sana kuhusu wakati ujao. Na hapo ndipo tunapaswa kufikiria juu ya hazina itakayotusaidia katika wakati huo. Kumbuka kuwa kwa kila anayeyafikiria Maisha yake wakati ujao ni lazima ajitaabishe katika wakati uliopo ili kuweka hazina. Nikukaribishe katika kitabu hiki ambapo mwandishi unazungumza kwa undani mambo ambayo yataiongeza nuru akili yako kwa habari ya Hazina Yako na Kizazi Chako. Karibu sana na Mungu akubariki. Ninaamini kama utakisoma kitabu hiki kwa kumaanisha na kwa umakini, basi Maisha yako hayatabaki kama yalivyo kiroho na kimwili.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza