HATIMA ILIYOFUTIKA
Hapa ulimwenguni kila mwanadamu ana ndoto kuu moja daima, nayo ni kuishi maisha yenye furaha na amani, na kila mtu huwa ana mambo yake mahususi yanayomletea furaha na amani maishani, hapo ndipo kila mmoja hujipambanua na kuweka malengo bayana juu ya kujipatia furaha na amani. Matokeo huwa ni mawili, aidha kupata yale anayoyatamania au kukosa kabisa, na hiyo ndio huitwa HATIMA. sasa inakuaje pale ambapo hatima ya mtu inafutika, je mtu huweza kuipambania tena HATIMA ILIYOFUTIKA??.
Kila mwanadamu ana hatima ya pekee kwenye maisha yake ingawa maisha ni fumbo. Fumbo la kudra za Mwenyezi Mungu juu ya mja katika kipindi cha hai wake, na vichwani mwetu huwa tuna picha fulani ya hatima tunayoitarajia katika maisha yetu. Lakini kadiri maisha yanavyozidi kuendelea vitu viwili hutokea. Aidha ile hatima tarajiwa hufutika au la hujichora ikijidhihirisha zaidi na kisha hutimia. Fuatilia ujionee mapenzi kama sehemu ya maisha ya vijana wawili (Pozo na Kudrat) yanavyoathiri hatima yao, zaidi ni juu ya mazingira wanayopitia na kuzuka kwa janga
la mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO - 19).