
Hatari Na Hasara Za Kurudi Nyuma Na Kuacha Wokovu
Kitabu hiki kimeandikwa maalumu kwa watu wanne ambapo wewe ni mmojawapo,Wa kwanza ni yule ambaye amerudi nyuma na ameacha wokovu,kwenye kitabu hiki kuna sauti na wito wa Roho Mtakatifu juu ya hatua uliyonayo sasa lakini pia maarifa ya kukusaidia kurudi kwenye heshima uliyopewa na ufalme wa Mungu.Wapili ni kwa wewe ambaye biblia inakuita siyo moto wala baridi,huna uhakika wa mahali ulipo katika imani kama bado upo kundini au ulishatoka,kwenye kitabu hiki kuna sauti ya Mungu ya kukuvuta zaidi kwenye uhakika wa wokovu.Mtu wa tatu ni kwa wewe mwenye uhakika wa nafasi na hatua uliyonayo katika imani,wewe pia kuna maarifa ya kukusaidia ili kupambania imani nafasi na heshima uliyonayo katika ufalme wa Mungu mpaka mwisho,kumbuka mwisho mwema ni bora kuliko mwanzo mwema.Mtu wanne na wa mwisho niliyekuandikia kitabu hiki ni kwa wewe ambaye hujaokoka,Yesu kwako bado hana nafasi na heshima anayostahili kibiblia,hata wewe una sehemu yako katika andiko la kitabu hiki ili kukusaidia kuitikia wito wa Yesu msalabani.
Wokovu ni mfumo maalumu wa ki-maisha ulio asisiwa na kuratibiwa na Mungu mwenyewe katika hatua na itifaki zake zote tangu kizazi cha kwanza cha Biblia.
Tangu kuasisiwa kwa injili na kuthibitishwa kwa kufufuka kwa Yesu,hata sasa, kasi ya kuhubiriwa kwa injili kumeongeza matokeo ya watu wengi kuamini na kuokoka.Waamini wamekuwa wakiongezeka,kanisa limeendelea kukua na kuimarika ikiwa ni matokeo ya agizo la kuhubiriwa kwa injili ya Yesu Kristo katika kila pembe ya dunia.
Lakini pamoja na uzuri na uthamani wa wokovu,bado kuna waamini wamekuwa wakirudi nyuma na wengine hata kuacha kabisa wokovu pasipo kujua madhara na hasara inayotokana na hatua hii.
Kimsingi kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya kubainisha hatari na hasara anazo kabiliana nazo mwamini anayerudi nyuma na yule aliye acha kabisa wokovu.
Lakini pia katika kitabu hiki utajifunza kujua dalili za awali,za ndani za kuangalia kama umeanza kupuyanga kwa kurudi nyuma na kuacha wokovu.
Zaidi utajifunza juu ya hatua za kuchukua endapo umerudi nyuma au umeacha wokovu
Muhimu zaidi utajifunza juu ya hatua na itifaki za msingi za kuzingatia ili kutunza taji la wokovu na kukwepa hatari na hasara nilizozibainisha.
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; (Wafilipi 1:6) |
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza