Hadithi Za Mjini
MAISHA YA MJINI NA KUISHI KIMJINI MJINI
Alitembea na kuangalia mbele, alionak undi la vijana wakiwa wana vifaa vya kazi wakichimbua mfereji, walikua wengi hasa! Akajua wakisikia tu anaitwa lazima watamsimamisha, na wakijua kua ni mwizi kifo kitakua karibu zaidi ya uhai! Zumari akaona ni bora akajisalimishe kwa migambo kuliko kukamatwa na mwenye mali au hao vijana waliokua mbele yake. Akatazama na kuona hakuna magari. Akavuka na kuwafata wale migambo waliokua na watoto wa kiarabu. Alipowafikia akataka kuwasalimia lakini sauti haikutoka, akilini alianza kupanga kuwaambia kwamba aliona ule mzigo ukiwa chini akajua hauna mwenyewe ndio maana akachukua ili akawape watoto wale nyumbani. Akakohoa kusafisha sauti yake. Yule mtu aliyekua nyuma anae akawa kavuka kamfikia, akaongea huku akiwa anahema kwa nguvu.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza