
GOMA MAGOTINI
Kitabu Cha kukonga nyoyo!
GOMA MAGOTINI
MTOTO WA NYOKA NI NYOKA. Hivi ndivyo unavyoweza kumzungumzia Biruse, kijana machachari na hatari akiwa nyuma ya mtutu wa bunduki ama mbele ya adui.
Kijana huyu, ambaye ni mtoto wa kuzaliwa wa kachero maarufu na mwenye heshima kubwa kwenye medani za usalama Afrika, Othuman Seyunguson, akiwa kijana mdogo, lakini hatari; anapendekezwa na wakuu wa usalama Tanzania kwenda kwenye misheni ya ‘kuuza roho’ ya kupambana na mtandao wa Goma Cartel, uliokuwa unamaskani yake huko Goma nchini Kongo.
Mtandao huu hatari uliundwa na watu mashuhuri; ambao ni wanasiasa, wafanyabiashara, viongozi wa dini, n.k, waliokuwa na kazi kubwa mbili; kuchochea vita, machafuko na kupanda viongozi katika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye nchi za Afrika Mashariki kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
Misheni hii ni ya kufa ama kupona. Kwenda na roho katika mapambano na mtandao huu wa Goma Cartel lilikuwa ni jambo la kawaida, lakini kurudi nayo ulikuwa ni muujiza.
Katika safari hii, Biruse anapewa mshirika, mwanadada Sasha, kutoka Kenya, binti wa Farida, mwanausalama aliyeshirikiana kwa ukaribu na Othuman Seyunguson, katika misheni ya ‘oparesheni Khartoum 01’
Je, nini kitajiri kwenye misheni hii?
Fungua kurasa za kitabu hiki; visa na mikasa, mpangilio wa matukio, na kila kilichoandika vitakuacha kinywa wazi!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza