GHARAMA ZA UONGOZI
Ukiwa kiongozi kuna bei na gharama za kulipa. Haijalishi wewe ni kiongozi wa kiroho, wa kisiasa, wa kibiashara, au kifamilia gharama za kulipa hazikwepeki. Haijalishi unaongoza taasisi au kampuni, uwe unaongoza watu wengi au wachache bado gharama za uongozi zipo. Kila kitu kinakuja na gharama! Inaweza kuwa ni gharama ya muda, fedha, nguvu, hisia, usingizi, n.k. Huwezi kuwa kiongozi pasipo kulipa gharama. Viongozi wote wakuu katika Biblia kuanzia Musa mpaka Paulo walilipa gharama katika uongozi wao. Mafanikio hayawezi kupunguzwa bei, ukitaka mafanikio katika eneo lolote lazima ulipie gharama husika. Watu wengi tunataka nafasi za uongozi kwa ajili ya kupata heshima na umaarufu, na huwa tunazigombania bila kujua kuwa zipo gharama husika ambazo lazima mtu apitie katika mchakato wa kufanyika kuwa kiongozi. Ni vizuri kuzijua mapema ili kujiandaa kuzilipia pale itakapotakiwa kufanya hivyo. Viongozi wengi hawajui gharama za uongozi, wanaingia katika uongozi bila kuhesabu wala kujua, baadaye gharama zinapoanza kudai kulipwa wanachanganyikiwa.
GHARAMA ZA UONGOZI NI KITABU BORA CHA UONGOZI AMBACHO KINA MWAANDA KIONGOZI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBLI KATIKA UONGOZI WAKE. KATIKA UONGOZI KUNA GHARAMA MBALIMBALI ZA KUZILIPA, KITABU HIKI KIMECHAMBUA KWA KINA AINA MBALIMBALI ZA GHARAMA AMBAZO KILA KIONGOZI ANAYETAKA KUFANIKIWA NI LAZIMA AWE TAYARI KUZILIPA.