
Furaha Yako Haita Potea Tena
Zijue hisia 12 zinazoiba furaha yako na namna ya kuzikabiri
Je, unajua kuna hisia ambazo zinakuibia furaha kila siku bila hata wewe kugundua?
Ushawahi kujikuta ukiwa mwepesi wa kukasirika, kuumizwa, au kukata tamaa?
Kama jibu ni ndiyo, basi kuna jambo unapaswa kulifahamu ili kutoka hapo...
Kuna hisia ulizipa nafasi bila wewe kujua na zikaingia ndani yako zikajenga ngome na kuanza kukuendesha, hata leo bado umeziruhusu na umezipa nafasi.
Zimechukua nafasi kubwa kiasi kwamba hata haujui namna ya kuzidhibiti, zinakuendesha, zenyewe ndio zinakuamlia uwe na huzuni kwa muda gani au ufurahi kwa muda gani?
Zenyewe ndio zinakukuamlia uumie kwa kiasi gani haijalishi ukubwa wa tatizo uliokutana nalo, linaweza kuwa dogo tu lakini wiki nzima ukajikuta hauna furaha. Na pia ndio zinakulazimisha ujione wathamani kiasi gani.
Hujawahi kuona kuna muda ni kama haujielewi unasema sina mood hivi!
Wakati mwingine unaumia tu na maisha ya wengine bila sababu, basi tambua hizi hisia zipo kazini, actualy hizi hisia ni kama magugu ambayo hayapandwi lakini yanaota, na usipo yashughurikia kuyaondoa utapata hasara ya kutopata mavuno mazuri.
Ukweli ni kwamba furaha yako haijapotea ila imefichwa na hisia hizi, ukizishughurikia basi utaiona tena furaha yako na hautakuwa mtumwa tena wa huzuni.
Nimekuandalia kitabu hiki kwa ajili ya kukusaidia, Ukimaliza kusoma kitabu hiki utapata vitu vya kukusaidia katika kila hali unayopitia, furaha yako haiwezi kupotea, kumbuka furaha yako ndio nguvu yako.
Vitu vingi vizuri huwa vinakuja ukiwa na furaha,na pia furaha inanguvu ya kukusaidia kufanya chochote cha maana kwenye maisha yako, furaha ni nguvu ya kuvuta mafanikio.
Furaha ni kila kitu,kwa sababu wengi wanafanya kila kitu sio kupata fedha no! Ila kupata furaha.So hata fedha haina nguvu kama iliyobebwa na furaha.
Kitabu hiki kitakusaidia kuliko unavyodhania.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza