FUNGUO 5 ZA MAOMBI
Price:
7,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 23, 2024
Product Views:
729
Sample
Mambo 5 ya kuzingatia ili kuwa mwombaji mwenye mafanikio.
FUNGUO 5 ZA MAOMBI ni Kurasa 203 zinazofunua siri ya mafanikio kupitia njia ya maombi.
Inawezekana umekuwa ukiomba bila kupata majibu ya maombi yako. Au umekua hujui siri ya kufanikiwa kwako. Usijali suluhu imepatikana nayo imefunuliwa ndani ya kitabu hiki.
Usichokijua ni kuwa huwezi kufanikiwa nje ya mifumo ya kiroho. Mafanikio ya Mkristo yamefichwa kwenye mahusiano yake na Mungu. Na namna pekee ya kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ni kwa njia ya maombi.
Maombi ni njia ya kumfikia Mungu mwenye majibu ya maswali na shida zetu. Kadri tunavyo zidi kuomba ndivyo tunavyozidi kumsogelea na kadri tunavyozidi kumsogelea ndivyo tunavyozidi kuwa na mahusiano naye na kupata mahitaji yetu kutoka kwake.
Kama vile ambavyo huwezi kufanikiwa kwenye nyaja yeyote ya maisha pasipo kufahamu mbinu za eneo unalotaka kufanikiwa kwalo ndivyo ambavyo huwezi kufanikiwa kuwa mwombaji mweye mafanikio kama haujui siri ya kujibiwa maombi yako. Mlango upo mbele yetu, umeandikwa \"Ombeni nanyi mtapewa, Mathayo 7:7a\" na maneno ya msisitizo yamewekwa mbele yake \"Kwa maana kila aombaye hupokei Mathayo 7:8a\" sauti inasikika kutokea ndani ikisema \"Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu, Wafilipi 4:6. Wengi wetu tumeishia kuutazama mlango huo na kuondoka maana hatujui kilichomo ndani yake, na wengine wameishia kuusukuma kwa nguvu ili ufunguke bila mafanikio.
Maombi ni mlango wa kuingilia kwenye hazina ya mbinguni na ndani yake ndipo kwenye kila jawabu la mwanadamu. Lakini ili uweze kuingia kwenye hazina hiyo unapaswa kuwa na ufunguo sahihi wa kufungulia mlango wa kuingilia ndani ya hadhina hiyo ya thamani.
Kupitia maombi unaweza kupakuwa/ku- download (ndoa, mtoto, amani, biashara, fedha, kazi, afya n.k). Lakini kama hujui namna ya kupakua unachokitaka utaomba sana bila matokeo. Kuna hatua 5 za kuzingatia ili kuweza kupakua chochote unachokitaka kutoka kwenye ulimwengu wa roho na kukileta kwenye ulimwengu wako.
Pakua kitabu cha FUNGUO 5 ZA MAOMBI ili uweze kurahisisha safari yako ya mafanikio.
Johanes J Ryoba (0714054430)
Mwandishi
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza