Best Seller
FUNGUA UWEZO WAKO
Price:
7,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Nov 18, 2022
Product Views:
1,659
Sample
Ndani yako kuna UWEZO mkubwa sana. Uwezo ambao ikiwa utautambua na kuanza kuutumia basi utainuka juu kabisa kwenye eneo lako. Mungu hajakuleta hapa duniani ukiwa kama ombwe ndani yako ameweka uwezo mkubwa. FUNGUA UWEZO WAKO.
Hakuna aliekuja duniani akiwa mtupu, kila mtu alikuja duniani akiwa na uwezo mkubwa ndani yake. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi wanaishi chini ya uwezo wao.
Tafiti za kisayansi kwenye eneo la uwezo wa binadamu zinaonesha 90% ya uwezo wa binadamu hufia ndani yao, ni 10% tu ya uwezo huo hutumiwa.
Hii ni kwa sababu watu wengi hutumia muda mwingi kujilaumu kwa vitu ambavyo hawana na makosa waliofanya badala ya kujikita katika kutumia vile walivyonavyo. Wengine hujutia jinsi walivyoshindwa, jinsi walivyokataliwa na vitu walivyopoteza kwenye safari yao, mwisho wanahitimisha kwa kujiona hawana uwezo tena wa kufanya jambo lolote na matokeo yake kuua uwezo mkubwa uliopo ndani yao.
Hivyo kitabu hiki kinakuja kukukumbusha kuwa una uwezo mkubwa ndani yako ambao unapaswa kuutumia kufanya mambo makubwa kwenye hii dunia.
Kitabu hiki kinakupa mwongozo wa jinsi ya kuufungua uwezo wako na kuishi ukuu uliopo ndani yako.
Ndani yako kuna uwezo mkubwa sana, usikubali ufie ndani yako. FUNGUA UWEZO WAKO.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza